NA KHADIJA KALILI, NAIROBI
Kuna usemi usemao nabii hakubaliki nyumbani, ndivyo usemi huo unavyojidhihirisha kwa Mtanzania Kiango Kipingu,
akiwa kocha mahiri wa kutumainiwa kwa Taifa la Kenya.
Tanzania pamoja na kutokuwa na idadi kubwa ya makocha
waliobobea katika mchezo wa Tenis, bado
ameshindwa kukubalika nyumbani na ujzui
wake, kwa sasa unawanufaisha Wakenya.
Bongoweekend Blog ilifanya mahojiano maalum na Kocha huyo kwenye
viwanja vya Lunar Park Jijini Nairobi mwishoni mwa wiki na kujinasibu kuwa anafanya
kazi zake za kufundisha kucheza mchezo huo jijini hapa kwa nafasi kubwa kiasi
kuonyesha kipaji chake.
Anajipambanua kwa
kusema kuwa yeye ni Mwalimu wa
kutumainiwa katika shule ya Tennis inayofahamika
kwa jina la ACE Tennis Academy analipwa mshahara mnono kutokana na kazi hiyo.
¨Katika shule hii ambayo licha ya wanafunzi wake kusoma
masomo mengina ya kawaida lakini ni maalumu kwa kusaka wanafunzi ambao wana
vipaji huku lengo kubwa likiwa ni kupata wawakilishi wa nchi katika michuano ya mchezo huu” anasema
Kipingu.
Akifananisha namna
nchi ya Tanzania na Kenya wanavyo uthamini mchezo huo anasema “hapa wameweka mfumo rasmi
wa kuandaa vijana wadogo wenye kipaji cha kucheza mpira wa meza pia
huandaa wachezaji wa timu ya Taifa katika ngazi za awali na hii shule
ninayofundisha ndiyo kinara katika kutoa
wachezaji wadogo lakini wenye
vipaji katika uchezaji¨ anasema.
Changamoto alizopitia
Kipingu anaweka wazi na kusema kuwa jambo kubwa lililomkimbiza nyumbani (Tanzania) ni ukata wa fedha na kutothaminika
kwa kazi yake licha ya kuwa na mchango mkubwa
alioutoa katika timu za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuvumbua na kukuza
vipaji vya mchezo huo.
Anasema aliingia Jijini hapa Januari 2015 hapo alipokelewa vizuri na kufanikiwa kusaini
makataba wa miaka mitatu wa kufanya kazi hiyo.
¨ Sababu kubwa iliyonileta hapa Nairobi ni kutokana na
jinsi wenzetu wanavyo wajali makocha tofauti na ilivyo nyumbani, kwetu
hawathamini michezo na hawajali kuwa
michezo ni ajira ambayo inaweza kumtajirisha mtu lakini huku wanaheshimu
utaalamu wa aina yeyote ambao mtu anao na kuuendeleza kama jinsi nilivyojionea kwangu mimi
nimethaminiwa ugenini na kudharauliwa nyumbani ¨anasema Kipingu.
Anaongeza kwa kusema kuwa tofauti iliyopo kati ya nchi mbili hizi ni kuwa
Kenya wamejiwekea utaratibu wa kumthamini
mtu na utaalamu wake pamoja kumpa moyo muhusika.
Anaongeza kwa kusema kuwa nchini Kenya wanaipa kipaumbele
kikubwa michezo na ndiyo sababu wamekuwa
wakiweza kupata medali nyingi kwenye michuano ya kimataia huku akitolea mfano
wa mchezo wa riadha ambao wamekuwa waking’ara kwenye mashindano mbalimbali.
Anakwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa alipokuwa nyumbani
Tanzania alikuwa ni Mtaalamu wa Ufundi
wa mpira wa meza katika Chama Cha Tanzania Tennis Association (TTA), pia
alikuwa Msimamizi wa kueneza mchezo huo
nchi nzima huku akiwa amevalia
kofia nyingine ya Kocha Mkuu wa Tennis Tanzania.
Anasema licha ya kujitolea kwa hali na mali lakini
alikuwa halipwi ujira wowote licha ya
kuwa TTA, walikuwa na mdhamini ambaye alikuwa akitoa fedha lakini wajanja wachache na wasiopenda maendeleo ya mchezo huo walikula fedha
hizo na hadi leo bado hajalipwa chochote.
Kipingu anaweka wazi kwa kusema kuwa wakati akifundisha
timu nyumbani Tanzania , aliweza kufanikisha
timu ya Taifa ya Vijana chini ya
umri wa miaka 16 kufanikiwa kuingia katika fainali za Afrika Mashariki na Kati na kuibuka katika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo.
“Mimi niliongoza timu hiyo hadi ikafanikiwa kushika nafasi ya pili lakini
sikulipwa chochote , na hakuna kiongozi yeyote aliyeonesha kujali jitihada
zangu katika kuifikisha timu kwenye
nafasi hiyo” anasema Kipingu.
Aidha anaongeza kwa kusema kuwa akiwa nchini Kenya
ameweza kupata mafanikio ya kuipeleka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 14
kushiriki kwenye mashindano ya dunia ya mchezo huo yatakayofanyika mjini Pendevo nchini Serbia.
¨Wakiwa katika michuano hiyo nchini Serbia timu ya tenis Kenya
itakutana na timu nyingine zinazo
shiriki michuano hiyo kutoka nchi
mbalimbali duniani” anasema Kipingu.
Anasema michuano hiyo
ya vijana wadogo hufanyika kwa
kuzingatia kalenda ya shule, michuano hiyo hufanyika wakati wanafunzi wamefunga
shule¨ anasema Kipingu.
Matarajio
yake katika siku za usoni
Anasema kuwepo
kwake nchini Kenya anajifunza mambo
mengi ikiwa ni pamoja na kuiba ujuzi
ambao amejipanga kuurudisha nyumbani Tanzania kwa lengo la kuukuza mchezo huo.
Najifunza sana kutoka kutoka kwa Wakenya, najifunza mawazo yao lakini bado pia
nina ndoto ya kurudi nyumbani ili kuukuza mchezo huu.
Anasema kuwa ana
ndoto ya kuja kuendeleza mchezo wa Tennis kutengeneza wachezaji ambao wataweza kupata ajira kwa kupitia
mchezo huo kwani michezo ni ajira.
Anasema hivi sasa
tayari ameshasajili Kampuni yake ambayo
pindi atakapokuwa tayari kurudi nyumbani atakuwa na mradi wa kusaka vipaji na kuviendeleza,nitakaporudi
nyumbani nitakua natafuta vipaji na kuaendeleza.
Nitakaporudi nyumbani nitanzisha shule maalum ya Tenis ambayo itatoa elimu na kuwafundisha vijana .
“Uzuri wa mchezo wa Tenis unaweza ukawa na vijana 50
ambao kati yao ukafanikiwa kuibua
mchezaji mmoja ambaye akaja kuwa nyota mmoja wa wataifa kama vile Serena
Williams alivyo tajiri kutokana na kupata mshahara mnono na kuingia mikataba
mingi ya matangazo ya biashara nina imani
katika hili Tanzania inaweza kufanikiwa
kuja kupata mchezaji atakayeng’ara kimataifa” anasema Kipingu.
Nasaha zake kwa serikali
Anazungumza huku akionesha msisitizo katika hili anaiomba serikali iliyopo madarakani hivi sasa itupie jicho la tatu kwenye sekta ya michezo
huku akiomba viongozi wa juu waweze kubadilishwa endapo tunataka
kufanya mapinduzi kwenye michezo.
“Mfumo tulioukuta na viongozi wa michezo kama vile Mkurugenzi wa Michezo
Leonard Thadeo angebadilishwa na nafasi
hiyo apewe kijana ili aje na mawazo mapya
itasaidia kuweza kubadili mfumo mzima wa michezo ambao hauna malengo yoyote ndiyo sababu kubwa Tanzania
hatufiki mbali kwenye michezo” anasema Kipingu.
Anaweka wazi kwa nini Thadeo abadilishwe ni kutokana na
kushindwa kuipeleka mbali michezo kutokana ubunifu wake wa mikakati ya michezo
kufikia ukomo.
“Mimi tangu nilipokuwa kijana mdogo namsikia tu lakini
sijaona matunda yeyote aliyoleta katika
michezo nchini” anasema Kipingu.
Anakwenda mbali
zaid kwa kusema katika michezo kuna
fedha na ajira za kutosha lakini jambo moja kubwa tunalohitaji ni
kujiwekea mikakati madhubuti ili tuweze
kuwafikia walipo wenzetu na nchi nyingine ulimwenguni.
Anasema yuko
tayari kufanya kazi na kocha yeyote
nchini ambaye atajitokeza ikiwa ni katika kuukuza mchezo huu.
Alikotoka
Anasema alipokuwa mwanafunzi alikuwa anapenda mchezo wa soka na alikuwa
akicheza kwa umahiri kipaji ambacho
kilivumbuliwa na kukuzwa na aliyekuwa
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kijeshi ya Makongo Kanali Mstaafu Idd
Kipingu ambaye ni baba yake mdogo.
Lakini alikuja kubadilika baada ya kumshuhudia kaka
yake anayemtaja kwa jina la Sebastian Mtupili aliyekuwa bingwa wa Tenis nchini katika miaka ya nyuma.
Jinsi alivyovutiwa na mchezo huo anasema ilitokana na
kwenda kuangalia mechi alizokuwa akilicheza kaka yake ndipo alipoanza kuupenda mchezo huo.
0 Comments