TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wanaharakati ngazi ya jamii kutoka maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Shinyanga, na washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Kikundi Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BATT) na Asasi nyingine za Kiraia wamefanya maandamano wakiwa wameshika mambango yenye ujumbe pamoja na kutoa tamko baada ya kufanya uchambuzi wa kina na kuainisha maboresho na mapungufu ya bajeti ya Taifa ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (MB) tarehe 08 Juni 2016 Bungeni Dodoma.Picha na Geofrey Adroph.
Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye maandamano
Mwanaharakati Nyanjura Kalindo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) akitole msisitizo kuhusu tamko lao lililotolewa kuhusu Bajeti ya Taifa iliyosomwa Jana Bungeni.
Mwandishi wa Channel Ten akiuliza swali kwa Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa mara baada ya kutoa tamko kuhusu Badger ya Taifa iliyo somwa Jana Bungeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akitolea ufafanuzi moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari.
Mwanaharakati kutoka Kigamboni, Bi. Subira Abdalah Kibiga akitolea ufafanuzi moja ya moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari wakati wanatoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari kuhusu Bajeti ya Taifa iliyosomwa jana Bungeni mjini Dodoma.
Mwanaharakati Selemani Bishegezi akijibu akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari
Baadhi ya Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bajeti ya Taifa iliyo somwa Jana Bungeni.
0 Comments