Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania Maharage Ally Chande pichani juu.
Kama mojawapo ya makampuni ya Afrika yanayoongoza
katika sekta ya burudani za video, MultiChoice inatambua kwamba rasilimali watu
ni kitovu cha simulizi ya mafanikio yake-ndio maana inawekeza sana katika
kutafuta, kuendeleza na kunoa watu bora kabisa katika sekta. Kama kampuni ya
kimataifa, falsafa yetu ya kufikiri kimataifa na kutenda kwa ndani ya nchi
inaungwa mkono na programu za kuendeleza utendaji wenye nguvu na sera ambazo
zimejizatiti katika kuendeleza biashara za ndani na kuajiri watu kutoka miongoni
mwa vipaji vilivyolelewa na kukulia nchini.
MultiChoice Tanzania inayo furaha kutangaza uteuzi wa
Bw. Maharage Ally Chande kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania.
Chande anajiunga na familia ya MultiChoice baada ya hapo awali kushika wadhifa
wa Mkurugenzi Wa Huduma Za Taasisi katika Ofisi Ya Rais-Ufuatiliaji wa
Utekelezaji wa Miradi
( President’s Delivery Bureau).
( President’s Delivery Bureau).
Mwenyekiti wa MultiChoice Tanzania, Bw.Ami Mpungwe,
akiidhinisha uteuzi huo amesema; “MultiChoice Tanzania inaona fahari kuhusu
uteuzi huu- hakuna shaka kwamba Bw.Chande ni miongoni mwa watanzania watendaji
bora kabisa na anakuja pamoja na uzoefu mkubwa katika masuala ya usimamizi wa taasisi. Sifa zake kama mtaalamu wa huduma za kibenki
na kifedha pamoja na tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ni ujuzi tunaouhitaji
katika biashara yetu ili kuipeleka biashara ya Tanzania katika viwango vipya
vya hali ya juu. Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya na bila
shaka atawahudumia wateja wetu wa DStv kwa nguvu na juhudi mpya.” Bw.Chande ni
mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu MultiChoice Tanzania.
Maharage amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za
kiutendaji kama Afisa Mtendaji Mkuu katika Benki Ya Taifa Ya Biashara(National
Bank Of Commerce) kampuni tanzu ya Barclays/ABSA-na pia kutekeleza majukumu ya
Meneja Mtendaji wa Tekinolojia na Mawasiliano, Data na Huduma za Ongezeko la
Thamani. Ana shahada ya Sayansi katika Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo
Kikuu Cha Dar-es-salaam na Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka
Chuo Kikuu Cha Afrika Kusini.
0 Comments