TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA MATOKEO YA AWALI YA URAIS YA MAJIMBO MATATU.
Na Lilian Lundo-Maelezo
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametangaza matokeo ya awali ya nafasi ya Urais katika majimbo matatu, ambapo majimbo mawili kutoka Zanzibar na jimbo moja kutoka Mtwara.
Jaji Lubuva alitangaza matokeo hayo baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 uliofanyika Oktoba 25. Aliyataja Majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Makunduchi na Paje yaliyoko Zanzibar na Jimbo la Lulindi lililoko Mkoa wa Mtwara.
Jaji Lubuva alitangaza matokeo hayo leo kwa waandishi wa habari wa kitaifa na kimataifa katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 4: 00 asubuhi.
Jaji Lubuva alisema katika Jimbo la Makunduchi CCM imeongoza kwa kura 8,406 sawa na asilimia 81.20 ya kura halali ikifatiwa na CHADEMA imepata kura 1,769 sawa na asilimia 17.09 ya kura halali, vyama vingine ni CHAUMA kura 68 sawa na asilimia 0.66 ya kura halali, ADC kura 58 sawa na asilimia 0.56 ya kura halali, NRA kura 23 sawa na asilimia 0.22 ya kura halali, ACT kura 22 sawa na asilimia 0.21 ya wapiga kura, TLP kura 18 sawa na asilimia 0.17 ya kura halali na UPDP kura 18 sawa na asilimia 0.17 ya kura halali.
Aliongeza kwamba katika Jimbo la Paje CCM imeongoza kwa kura 6,035 sawa na asilimia 75.00 za kura halali, ikifuatiwa na chama cha CHADEMA kilichopata kura 1,899 sawa na asilimia 23.60 ya kura halali, ACT kura 36 sawa na asilimia 0.45 ya wapiga kura, CHAUMA kura 28 sawa na asilimia 0.35 ya wapiga kura. TLP kura 08 sawa na asilimia 0.10 ya kura halali, NRA kura 08 sawa na asilimia 0.10 ya kura halali na UPDP kura 07 sawa na asilimia 0.09 ya kura halali.
Jimbo la Lulindi CCM imeongoza kwa kura 31,603 sawa na asilimia 71.28 ya kura halali, CHADEMA kura 11,543 sawa na asilimia 26.03 ya kura halali, ACT kura 528 sawa na asilimia 1.19 ya kura halali, ADC kura 362 sawa na asilimia 0.82 ya kura halali, CHAUMA kura 179 sawa na asilimia 0.40 ya kura halali, TLP kura 43 sawa na asilimia 0.10 ya kura halali, NRA kura 43 sawa na asilimia 0.10 ya kura halali na UPDP kura 34 sawa na asilimia 0.08 ya kura halali.
“Matokeo haya ni ya awali, tume inaendelea kutangaza matokeo ya majimbo mengine kadiri itakavyokuwa ikipokea matokeo kutoka majimboni” Alisema Jaji Lubuva.
Kwa mujibu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC, Ramadhani Kailima alisema tume hiyo itayatangaza matokeo ya Urais mara nne kwa siku, saa 4:00 – 5:00 asubuhi, saa 6:00 - 7:00 mchana, saa 9:00 – 10:00 jioni na saa 12:00 – 1:00 jioni mpaka majimbo yote yatakapokuwa yamekamilisha kutuma matokeo uchaguzi huo.
0 Comments