BONDIA VICENT MBILINYI |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini
mkataba wa kuzipiga na Deo Njiku wa Morogoro siku ya Desemba 25 katika
uwanja wa jamuhuri morogo wakisindikiza mpambano wa Fransic Cheka na
Thomasi Mashali mpambano uho wa raundi sita
utakuwa wa kwanza kwa bondia Mbilinyi
kucheza mkoa wa morogoro akizungumzia mpambano huo bondia huyo amesema
kuwa anamjua mpinzani wake vizuri kutokana na ukongwe wake kwa kuwa
alianza zamani kupigana ata hivyo mimi nina jiamini na nitamkalisha
katika raundi za awali
bondia huyo alieweka kambi yake mkoa wa pwani maeneo ya Kibaha ambapo ameweka kambi yake kwa ajili ya mpambano huo
bondia huyo anaefundishwa na Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi ncini Rajabu Mhamila 'Super D'
amejizatiti kumtwanga vizuri tu Deo njiku ili ajisafishie njia ya kuwa
bingwa wa mchezo wa masumbwinchini
nae
Kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D;' aliongeza kwa kusema kuwa ana
matumaini na bondia wake kwa kuwa na rekodi nzuri ya mchezo ambapo mpaka
sasa amecheza michezo 7 kashinda 5 droo 1 na kupoteza 1 kwa rekodi hiyo
bondia huyo ana uchu wa kubaki kileleni na kuendeleza kichapo kwa kila
bondia anaekutana nae
0 Comments