IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA VICENTI MBILINYI KUWAKABILI WAPINZANI WAO AGOST 22


Bondia  bingwa wa Afrika wa mikanda miwili WPBF na UBO Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe'anapanda tena uringoni kwa mara nyingine kukabiliana na Ally Muro katika mpambano wake  wa kumaliza ubishi nani zaidi kati ya mabondia hawo utakaofanyika katika viwanja vya basketball vilivyopo katikashule ya msingi Uhuru Wasichana Kariakoo Dar es salaam

bondia huyo mwenye historia ya kucheza machezo mzuri wa masumbwi misri ya mfalme wa ngumi duniani Mohamed Ali amekuwa kivutio kikubwa nchini ambapo mashabiki wengi wamekuwa wakimulizia kuwa anacheza lini hata hivyo jibu limepatikana kuwa anacheza agost 22 katika viwanja vya shule ya Uhuru wasichana

katika mpambano uho watasindikizwa na bondia machachali anaechipukia kwa sasa Vicent Mbilinyi atakayemenyana na Kelvin Majiba wakati Raymond Mbwago atacheza na Roger Masawe wakati Husein Pendeza atamalizana ubishi na Shomari Mirundi mipambano yote hiyo ni ya raundi sita
 lengo likiwa ni kuwashulisha mabondia wafanye kazi yao ya ngumi na kufanya mazoezi kila wakati ili mabondia hawo wapate chachu na changamoto za mchezo kila wakati ili waweze kupata mapambano makubwa ambaya yatawapeleka mbali zaidi kimchezo ambapo michezo yote itakayochezwa siku hiyo itawekwa katika madaraja mbalimbali ya viwango vya mabondia boxrec
Lengo  kubwa la mchezo huo ni kumpongeza Lulu Kayage bondia pekee wa kike katika ngumi za kulipwa aliyethubutu kuonesha uwezo wake akiwa ugenini na kumpiga kwa T.K.O ya raundi ya pili bondia wa Afrika ya kusini Lizbeth Sivhaga na ndie atakaekuwa mgeni wa heshima katika mapambano hayo
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile



Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi



pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Post a Comment

0 Comments