Mbunge
Joshua Nassar akiwa na mkewe Anande Nnko wakati wa sherehe ya kimila
iliyoandaliwa na wananchi katika jimbo la Arumeru Mashariki baada ya
kufanikiwa kumaliza mgogoro wa maji uliokuwepo katika baadhi ya vijiji
.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya
Kaskazini.
WANANCHI wa vijiji vya Leguruki na King’ori katika wilaya ya
Arumeru wameandaa sherehe kubwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Arumeru
Mashariki ,Joshua Nassar baada ya kutatua mgogoro wa maji uliodumu kwa muda
mrefu katika vijiji 15 vya wilaya hiyo.
Sherehe hiyo iliyoenda sanjari na shughuli za kimila
ilishuhudiwa
mbunge huyo pamoja na mkewe Anande Nnko
wakivishwa maazi ya kimila pamoja na kukabidhiwa rungu huku mkewe akikabidhiwa
kibuyu pamoja na ijiti cha kimila.
Uamuzi wa wananchi hao unatokana na Mbunge Joshua Nassar
kutatua mgogoro kwa kuunda timu ya viongozi wa Din,Mila,Vijiji na kuamua
kuwapeleka Dodoma na kukutana na Waziri wa maji,Waziri wa Tamisemi na Waziri wa
Nishati na Madini kwa ajili ya mazungumzo.
Safari ya viongozi hao ndio iliyozaa kuvunjwa kwa iliyojiita
bodi ya maji yaliyofadhiliwa na shirika la OIKOS East Africa kwa vijiji 15
katika wilaya hiyo huku ikiwalipisha wananchi kwa
lita.
Mbali na kutozwa fedha kwa wananchi hayo bodi hiyo pia
ilidaiwa kusababisha baadhi ya wananchi kuwekwa rumande kwa hila huku mbunge
huyo akipambana na kufanikiwa kuwatoa.
Katika sherehe hiyo viongozi wa mila na dini walimsimika
Nassar huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkno katika mapambano ya kupigania
wananchi wa Meru ili kuondokana na hali ya
umaskini.
Akizungumza katika hotuba yake ,Nassar alisema bodi ya maji
imevunjwa na kauli ya waziri wa maji ni "wananchi ndio wenye Mamlaka ya
mwisho kimaamuzi.
“Linapokuja swala la namna bora ya kuchangia na sio kulipia,
ikizingatiwa mradi huu ulijengwa kwa nguvu za wananchi bila malipo yeyote kwa
miaka 3 wananchi wanapaswa kupata huduma hii ya maji”alisema
Nassar.
Nassar alitumia sherehe hiyo kukabidhi magari ya kubeba
wagonjwa huku yakiombewa na kuwekwa wakfu ili yakawe sehemu ya uponyaji kwa
watu wa Arumeru Mashariki.
Wananchi wamekiri kwa umoja wao "hawajawahi kupata Mbunge
Kama Nassari baada ya Japhet Kirilo.
Mwisho.
|
0 Comments