TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko
kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na shirika la
Open Society International East Africa (OSIEA) na wasanii mbalimbali
wa muziki wamezindua kampeni maalumu ya kuwahamasisha vijana
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye
kupiga kura.
Kampeni hiyo imezinduliwa Jijini Dar es Salaam na inatarajiwa
kuhusisha mikoa mitano ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza,
Shinyanga na Morogoro ambapo yatafanyika matamasha mbalimbali ambayo
hayana viingilio na yatakayowahusisha wasanii walioteuliwa kama
mabalozi katika kampeni hii.
Kauli mbiu ya kampeni hii ni ‘Kura dili’ na lengo kuu ni kuhakikisha
vijana wengi iwezekanavyo wanajiandikisha na kujitokeza kwa wingi
kupiga kura.
Wasanii watano wametunga wimbo maalumu uitwao ‘Kuradili ambao pia
ulizinduliwa katika hafla hiyo na utatumika katika kampeni hii.
Wasanii hao ni pamoja na Gnako, Snura, Izo Biznez, Kala Jeremiah na
Stamina.
Akizungumza kwa niaba ya Masoko,mmoja wa wakurugenzi, Constantine
Magavila alisema kampeni hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya watu milioni
4 kujisajili na kupiga kura na watashirikiana na redio mbalimbali
kuhakikisha wimbo huo maalumu unapigwa katika redio mbalimbali ili
kuhamasisha zaidi.
“Tumegudua kuwa vijana wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana endapo
watajitokeza kupiga kura kwa wingi kwa hivyo tunaanza kwanza
kuwahamasisha wajitokeze kupiga kura na baadaye waende kupiga kura kwa
wingi,” alisema.
Alisema kampeni hii itahusisha mikoa mitano lakini wanaamini ujumbe
utasambaa Tanzania nzima ili vijana waweze kutambiua kuwa kura ni dili
kama kauli mbiu ya kampenihiyo inavyosema.
“Tunaamini kampeni hii itakuwa na mafanikio makubwa na uchaguzi wa
mwaka huu utavunja rekodi,” alisema na kuongeza kuwa watashirikiana na
NEC kuhakikisha hili linafanyika.
Naye mwakilishi wa OSIEA ambaye ni Meneja Mkazi, Agnes Hunt, ambaye
shirika lake lilisaidia katika kurekodi wimbo huo maalumu alisema kuwa
wanashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo yasiyo ya kiserikali
katika masuala ya uwazi na utawala bora.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Elimu wa NEC Kitaifa, Bi
Rose Mongi aliishukuru Kampuni ya Masoko kwa jitihada zake za
kuhamasisha vijana na kusema kuwa NEC haina fedha za kutosha hivi
inategemea makampuni kama haya kujitokeza na kusaidia wakati kama huu.
Alisema Masoko imepewa kibali ya kutoa elimu ya upigaji kura ikiwemo
uandikishaji katika daftari la wapiga kura.
“Unaweza kuhamasisha vijana kujiandikisha na wakafanya hivyo lakini
wakaacha kujitokeza siku ya kupiga kura…hii itakuwa kazi bure kwa
hivyo kampeni hii itasaidia kuwafikia hawa vijana na kuwahamasisha
wajiandikishe na pia wajitokeze kupiga kura,” alisema na kuwapongeza
wasanii wote walioshiriki katika jitihada hii.
Izo Biznez ambaye ni mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika kampeni
hiyo alisema, “Sisi kama wasanii tunashukuru kupata nafasi kama hii ya
kuongeana vijana na kuwahamasisha wajiokeze kujiandikisha na kupiga
kura ifikapo mwezi Oktoba.”

Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura ilijulikanayo kama 'Kuradili". Kampuni hiyo itafanya kampeni hiyo katika mikoa kadhaa kwa kushiriakiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki. Kulia ni mwanamuziki Sinura Mushi na kushoto ni Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwanamuziki Stamina, Kala Jeremia, Snura, Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo na Ofisa Mipango Msaidizi wa Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), Adam Anthony.
Mkutano ukiendelea.
Wanamuziki wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Stamina, Kala Jeremia, na Snura
Wanamuziki hao wakiimba wimbo maalumu walioutunga wa kuhamasisha kupiga kura kupitia kampeni yao ya KURAdili mbele ya wanahabari.
Na Dotto Mwaibale O712 -727062
Na Dotto Mwaibale O712 -727062
0 Comments