MRATIBU WA SASI YA BETTER LIVING AID ATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA


Watangazaji Hamisa Mussa Lubilo na Deogratius Yagomba wa VOT fm 89.0 wakimuuliza maswali mratibu wa asasi ya Better Living Aid walipomualika leo asubuhi katika kipindi cha Meza huru!
Mratibu wa asasi ya kiraia ya Better Living Aid Bw Mkala Fundikira leo akiwa amavalia fulana ya mkakati wa Imetosha unaopinga mauaji dhidi ya watu wenye ualbino ambao yeye ni mjumbe wa kamati kuu, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mjini Tabora waiunge mkono asasi yake inayodhamiria kujenga vyoo na zahanati katika kijiji  cha Amani kilichopo Ipuli Tabora, kijiji chenye wakazi wazee na wasiojiweza na waishio na gonjwa sugu la ukoma. Alitoa wito huo akiongea katika kipindi cha meza huru cha Vot fm89.0 alisema "nawaomba wenye maduka ya vifaa vya ujenzi watuunge mkono kwa kuchangia hata mifuko mitano ya simenti, bati mbili au hata kifaa chochote cha ujenzi ambacho kitataumika katika ujenzi wa vyoo na zahanati katika kijiji hicho alimradi tunahitaji michango ya aina yeyote ile" 
Mkala Fundikira akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na watangazaji wa kipindi cha Meza huru, kipindi kinachoruka ktk kituo cha redio cha VOT fm 89.0 ya Tabora leo asubuhi.
Pamoja na kueleza kuwa asasi yao inayoundwa na marafiki toka mitandao ya jamii kama Facebook  na Viber pia alieleza kuwa tangu waanze kusadia kijiji hicho washapeleka vyakula, vyandarua na masweta kwa nyakati tofauti, pia ikiwemo kulipia upulizwaji wa dawa za kuuwa wadudu pamoja na kunguni ambao walikuwa wakisumbua wakazi wa kijiji cha Amani. 
Mkala akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wenye kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino ya mkakati wa Imetosha.
Alipoulizwa dhamira ya asasa yao ni kusaidia Tabora tu au na mikoa mingine? Mratibu huyo alijibu "Hapana, Better Living Aid itasaidia na kwingineko pia, kwa mfano tunatafuta wahisani ili tukajenge zahanati kijijini Masweya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Masweya hakuna zahanati pamoja na kuwa pana wakazi zaidi ya 7000, nafikiri wa Tanzania tuwe wahalisia kuwa serikali yetu haitoweza kukidhi mahitaji ya wa Tanzania wote kwa wakati mmoja hivyo basi ni wakati muafaka wa sisi kama jamii kuanza kujitolea na kuwezesha asasi kama yetu kupeleka huduma za afya sehemu kama Masweya"

Fundikira pia alimshukuru Mh Munde Tambwe Abdallah kwa kutoa ahadi ya Mifuko 50 ya simenti, lori 10 za mchanga pamoja na tano za mawe na kokoto , alisema "Tena kabla sijasahau nimpongeze na kumshukuru sasa sana sana Mh Munde Tambwe kwa kutupa msaada ambao ni msingi, kwa maana ya kuwa ahadi yake ndiyo itaanzisha ujenzi wa majengo hayo ya vyoo na zahanati, hivyo basi na wengine wajitolee ili tusonge mbele" 
Hoteli ambamo chakula cha usiku cha uchangishaji fedha kwa ujenzi wa vyoo na zahanati utafanyika baadae mwezi huu jijini Dar es Salaam iliyopo maeneo ya Ocean road.
Aidha asasi hiyo ina mpango wa kuandaa chakula cha usiku jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Southern Sun baadae mwezi huu ambapo Mh Samuel Sitta(waziri wa uchukuzi) amekubali kuwa mgeni rasmi, karamu hiyo itaandaliwa ili kuchangisha fedha za kuwezesha miradi hiyo iweze kukamilika. "Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za maandalizi lakini tunataraji karamu hiyo ya uchangishaji pesa ifanyike ama mwishoni mwa mwezi wa MEI au mwanzoni mwa mwezi Juni 2015. Pia Fundikira aliwashukuru Mh Aden Ragen(Mbunge wa Tabora mjini), Mh Munde Tambwe(Viti maalum), Sylvester Koka(Mbunge wa Kibaha) na wanachama na wote wa Better Living Aid kwa kuwezesha kifedha upulizwaji wa dawa kijiji cha Amani uliogharimu Tsh Laki 980.

Tembelea mtandao wa betterlivingaid.Blogspot.Com ujue zaidi kuhusu asasi hii na malengo yake au piga namba 0754 666620 kwa maelezo.

Post a Comment

0 Comments