Social Icons

Saturday, May 2, 2015

TSHIMANGA KALALA ASOSA APANIA KUWA MWALIMU WA LINGALA

MWANAMUZIKI  Mkongwe Tshimanga Kalala Assosa wa kwanza  kushoto pichani juu Jumapili hii May tatu 2015, atazindua kitabu chake  kinachopatikana katika lugha ya Lingala kilichokuwa kikisubiriwa  kwa hamu  na watu wengi sana kwa muda mrefu.
Uzinduzi huo ambao umepangwa  kufanyika katika ukumbi wa  MRC  kuanzia saa 12 jioni hadi saa  tatu ambako pia kipindi cha 'Club Raha Leo Show' kinachorushwa na luninga  ya TBC1 kitakuwa kikiendelea.Kitabu hicho ambacho kinaenda kwa jina la 'Jifunze Lingala  kwa Kiswahil'.
 
Aidha uzinduzi huo utakwenda sambamba na Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni.
Assosa aliwahi kutamba na bendi  kadhaa barani Afrika ikiwemo  Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka bendi zote hizi ni za Jamhuri ya Kidemrasia ya Kongo (DRC) .
 
Mara alipoingia nchini alifanya  kazi na  bendi ya Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Marquis.

No comments:

 
 
Blogger Templates