Marehemu
Komba aalimpigia simu Abdul Misambano mwimbaji wa taarabu ambaye aliweza
kufahamika kwa jina la ‘Asu’ kutokana na kibao chake amvcho hata kikipigwa leo
bado kitaamsha hisia za msikilizaji.
Komba
alimpigia simu Misambano na kumsisitiza aende mazoezini kadhalika alifanya
hivyohivyo kwa Thabit Abdul ambaye ni kati ya wapiga kinanda mashuhuri nchini
wote kila kila mmoja alimtumia fedha kwa
njia ya Tigo Pesakiasi cha sh. 100,000 ambazo marehemu alisema watumie kama
nauli zao wanapokwenda mazoezini.
Lakini kabba
wasanii hao hawajazitoa wala kuzitumia ndipo ghafla wakapata taarifa kuwa
Mkurugenzi Komba wao amefariki
dunia na mazoezi hayakufanyika tena.
Aidha hakuna
mtu aliyetarajia kama Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Twanga Pepeta (ASET), Asha Baraka ndiye aliyeandika mashairi ya
wimbo ule ambao uliimbwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa Komba.
“Mimi nilikua
katika Kamati ya burudani ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mmoja wa Wakurugenzi wa
Clouds Media Ruge Mutahabapia hivyo nikapewa jukumu la kuwakusanya wasanii ili
waweze kutunga wimbo wa kuimba siku ya kuuga mwili wa marehemu komba” anasema
Asha.
Anaendelea
kwa kusema kuwa lakini mara baada ya kuona wasanii wanasumbua akaamua kuutumia
wimbo wa marehemu Komba aliouimba katika msiba wa Hayati baba wa Taifa Julius Nyerere kwa kutoa sifa zilizokuwa zikimuhusu Nyerere
na kumtaja Komba.
Hivyo
nikawambia wasanii wakiongozwa King Kiki ‘Wazee Sugu’ wasiumize sana vichwa vyao
kwa sababau wanaweza kukopi nyimbo za Komba kwa ni nyingi.
Hivyo baada
ya yeye kuandika mashairi hayo na
kumwonyesha Ruge akayakubali wasanii
wakafanyia mazoezi na kuingia studio, ambapo gitaa la rhythm na solo lilipigwa
na Miraji Shakashia wa Twanga Pepeta huku sauti ya kinanda ikiingizwa na Abdul
Salvador (Father Kidevu)pamoja na Nape
Nnauye (CCM).
“Hilo
lilikwa ni wazo langu hivyo ndiyo sababu kubwa iliyopelekea wasanii kutotunga
wimbo mpya wa kumuenzi Komba hivyo wakaamua kuupa jina la ‘Nani Huyo’ ”anasema
Asha.
Asha amefunguka zaidi namna walivyofahamiana na Komba katika enzi za uhai wake.
Asha anaaza
kwa kusema “mimi nilifahamiana na Komba mwaka 2000 ambapo Komba aliniandikia
barua ya kumuomba aliyekuwa mwanamuziki
wa Twanga Pepeta kwa wakati huo Ramadhani Masanja (Banzastone).
“Nakumbuka wakati
huo nchi ilikuwa katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu hivyo nilienda ofisini
kwake TOT CCM Mwinjuma Mwananyamala, Jijini Dar es Salaam tukakubaliana amchukue Banzastone na mara baada ya kampeni
atamrudisha twanga lakini hakurudi”.
Anaongeza
kwa kusema kuwa Banza akachukuliwa kwa dau nono na
kutokana na kukaidi kwake kumrudisha tukaingia kwenye mgogoro lakini
baadaye tukaja kuzunguma yale ya kaisha na kazi zikaendelea kama kawaida.
Asha
anaendelea kwa kusema kwamba nakumbuka Komba ndiye aliyechangia kuupandisha
muziki wa dansi nchini ambapo walikuwa wakifanya kazi kwa ushindani katika muziki, huku wote wakiwa kitu kimoja
katika kufanya kazi ambapo kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja wakakubaliana
kuandaa mpambano wa nani zaidi kati ya TOT na Twanga huku mpambano huo ukiwa
wenye kuvuta hisia za mashabiki wa wadau mbalimbali wa muziki wa dansi na wa bendi hizo mbili.
Asha
anasimulia kwamba onyesho hilo kubwa lilifanyika kwenye ukumbi wa Vijana Hostel
Kinondoni.
Asha anasema
uhusiano wao mzuri ulidumu hata baaada ya kuingia kwenye ulingo wa siasa ndani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo walikuwa wakikutana katika chaguzi
mbalimbali za kisiasa.
Asha
anaongeza kwa kumwelezea Komba kwa kusema kwamba hawakuishia hapo tu bali wao Twanga wakawa
wanapata nafasi ya kuomba jukwaa na hata vyombo vya TOT pale walipoomba kutumia huku marehemu
akimwambia asha atafute usafiri wa kubebea vifaa hivyo.
Kama hiyo
haitoshi Asha anasema kwamba ana siri nzito aliyoachiwa siku chache kabla ya
kifo cha Komba .
“Siku chache
kabla hajafariki marehemu Komba tulikutana soko la TX Kinondoni hivyo alifurahi
kuniona pale na kuingia katika gari langu hapo ndipo tulipozungumza mambo mengi
saana huku yeye akiwa ni mzungumzaji zaidi ambapo alianieleza matatizo yake na changamoto
nyingi anazokutana nazo na jinsi anavyokabiliana nazo, tulikaa kwenye gari
yangu tukazungumza ila kilichotukatisha
ni kukatika kwa mafuta ya gari hivyo AC
ikakata akanipa sh. 20,000 ili nimtume kijana na kidumu akaninunulie mafuta tukaachana hapo baada ya siku chache
kupita Jumamosi Februari 28 alasiri ndipo nikapigiwa simu kafariki dunia
nimeumia sana” anasema Asha.
Mbali ya
kuzungumza na marehemu siku chache na za
mwisho za uhai wake Asha anasema kwamba atapata taabu kwa mazoea aliyokuwa nayo
walipokuwa kwenye vikao vyao vya Kamati
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi NEC (CCM),Dodoma ambapo wajumbe wa mikoa
ya Ruvuma na Kigoma hukaa karibu hivyo atakapokiona kiti cha marehemu Komba
kitambumbusha namna alivyokuwa mcheshi wakati wa kikao kikiendelea na
walivyokuwa wakitaniana.
“Nakumbuka
mara ya mwisho katika kikao cha NEC ,Dodoma aliniita akanieleza matatizo yake lakini hayo ni siri yangu mimi”
anasema Asha.
Nitakapoingia
katika ukumbi nitakiona kiti chake roho
itaniuma sana sababu tulikua tunakaa
karibu hivyo nafasi yake nitaiona imepwaya ndani ya ukumbi.
Akimzungumza
kwa upande wa burudani anasema marehemu Kapteni Komba TOT ameandika historia ya
bendi hiyo kwa kuiendesha kwa umakini wa hali ya juu .
Hilo
lilijidhihirisha kwa jinsi alivyofanikiwa kuendeleza muziki wa taarab, kwaya na
muziki wa dansi.
“Pia Komba
alikuwa na vikundi vingi vidogovidogo ambapo vijana walikuwa wakikusanyika na
kuonyesha vipaji vyao ambavyo baadaye viliendelezwa” anasema Asha.
Anaongeza
kwa kusema kuwa katika kuonesha kwamba yeye hana ubaguzi aliweza kuwaajiri
wacheza shoo wenye ulemavu wa miguu ambao nao hawakufanya ajizi pale walipopewa
nafasi walicheza vizuri mtindo wa ‘Achimenegule’.
Asha anatoa
angalizo kwa uongozi wa CCM ambao ndiyo wanamiliki kundi la TOT, kwa kusema
kwamba anawaomba wafanye uteuzi kwa mtu mwenye
moyo ili aweze kuendeleza mema yote yaliyoanzishwa na Marehemu komba.
“Komba
alikuwa jabali nani asiyemtambua kwani
hata watoto wadogo walifanikiwa kuziimba nyimbo za TOT kwenye michezo yao kama
vile achimenengule”anasema Asha.
Naye
mwanamuziki Kalala Junior anavyo mlilia Kapteni Komba ambaye kwa sasasa ni mwanamuziki wa bendi ya
Twanga Pepeta anasema kuwa Kapteni Komba alikuwa ni kama baba yake kwa sababu
hata wakati akiitumikia bendi ya TOT alimchukulia kama mtoto wake na yeye akijiona kana kwamba yuko kwa babake
mzazi.
“TOT ilikuwa
bendi yangu ya pili hivyo sikuona taabu yeyote kuwa katika bendi ile kwani
nilikuwa bado kijana mdogo (20) kwa wakati huo” anasema Kalala.
Kalala
aliongeza kwa kusema kuwa amepata pigo kubwa sana lakini hakuna njia ila
kumshukuru mungu kwa kila jambo.
“Kapteni
Komba alikuwa ni mshauri wangu mkuu katika maisha yangu na kila wakati nilikuwa
napita TOT kumsalimia na kuchukua busara zake”anasema Kalala.
Anaongeza
kwa kusema kuwa hata alipokuwa akihama hama bendi alimsema hivyo aliposikia amerudisha
mizigo yake katika bendi ya Twanga Pepeta akamwambia nilijua huko kote ulikuwa
ukihangaika tu sasa hapo utulie.
Naye Mchumi
wa Wachumi wa Wilaya ya Kinondoni Yusuphred Mhandeni ambaye pia ni mdau mkubwa wa bendi za muziki
wa dansi hapa nchini aliongezea kwa kusema kuwa msiba wa Komba ni pigo kwa
taifa kwani Komba amechangia katika kukuza muziki wa dansi nchini na kuufikisha
hapa ulipo sasa.
Kama
itakumbukwa Komba ndiye aliyeanzisha mtindo wa kununua wanamuziki kwa bei ya
juu hivyo hadi hapo utaona aliupa hadhi muziki nz wanamuziki pia .
“Aliweza
kuwaajiri TOT kwa nyakati tofauti
wanamuziki wakubwa watatu ambao ni mafahari watatu kama Banzastone, Ally Choki na Muumini
Mwinjuma” anasema Mhandeni
Muziki wa
dansi una vipaji vitatu ambavyo ni Muumini, Choki na Banzastone wote hawa Komba
aliweza kuwamiliki .
Mhandeni
anamalizia kwa kusema kuwa siyo siri kwa upande wa siasa CCM wamepata pigo
kwani Komba alikuwa na kipaji cha kuhamasisha katika kampeni.
Tumepoteza
kipaji ambacho kukipata itakuwa kazi na labda mtithi wake atazaliwa na vizazi
vijavyo siyo sasa.
Mwisho.
Mwandishi wa
makala hii anapatikana kwa Email :lindashebby@gmail.com 0755707046
0 Comments