Afisa
wa Kanda ya Afrika wa ICAO Papa Issa Mbengue (kushoto)akisisitiza
jambo juu ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga
(ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya
usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege wakati wa
Kongamano la mafunzo ya ufanisi wa masuala ya uongozaji wa ndege
linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
kwa udhamini wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) Charles Chacha(watatu kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia) Meneja mratibu wa
safari za ndege Afrika Frederic Legrand. (wapilia kutoka kulia) na
Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don
Facpues Ould.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles
Chacha(kushoto) akiongea wakati wa uzinduzi wa kongamano la mafunzo ya
mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye
kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa
anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege katikati ni Meneja mratibu wa
safari za ndege Afrika Frederic Legrand, Kongamano hilo linazihusisha
nchi za Afrika linafanyika hapa nchini kwa siku tatu kuanzia leo katika
hateli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma
za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia)
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles
Chacha akimsikiliza kwa makini Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika
Frederic Legrand(African Flight Proceducare Manager) wakati alipokuwa
akizungumza kwenye kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la
Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa
kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya
kuongonzea ndege.Kongamano hilo la siku tatu katika hateli ya Serena
jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa TCAA.
Baadhi
ya washiriki wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la
Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa
kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya
kuongonzea ndege,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa hapo
kongamano hilo limedhaminiwa na TCAA.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles
Chacha (kulia)akisalimiana na Makamu wa rais wa airspace and airlines
Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould, baada ya kufungua
kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa
Anga (ICAO) lenye ufanisi wa kulenga wataalamu wa kuongoza ndege
,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea
ndege.Kongamano hilo linafanyika kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli
ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja mratibu wa safari za
ndege Afrika Frederic Legrand.(African Flight Proceducare Manager)
Washiriki
wa kongamano lamafunzo ya mfumo mpya wa shirika la kimataifa la usafiri
wa anga (ICAO)kutoka nchi za Nigeria,Mali,Ivort
coast,Senager,Rwanda,Cape Verde,Gabon na Tanzania wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wa Kongamano hilo la siku tatu linalofabnyika kwenye
hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
0 Comments