Wajumbe
kutoka shirika la afya ulimwenguni wanakutana Geneva Uswis kuamua iwapo
wautangaze mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kama janga la barani Afrika na
dharura ya dunia.
Mkutano huo unakuja wakati raia mmoja wa Saudia Arabia amefariki akiwa na dalili za ebola katika mji wa Jeddah.
Iwapo
itathibitika msaudia huyo amekufa kwa ebola, kitakuwa kifo cha kwanza
nje ya bara la Afrika kusababishwa na virusi vya Ebola. Arnold Kayanda
na maelezo zaidi.
Tayari
ugonjwa huo ambao umeenea zaidi katika eneo la Magharibi mwa Afrika
umeshaua zaidi ya watu 900 kwa mwaka huu na unaonekana kuenea kwa kasi
katika maeneo mengine baraani humo.
Vifo
hivyo pamoja kasi ya kuambukiza huenda ikiwa kichocheo cha kulifanya
shirika la Afya duniani kutangaza ugonjwa huo kuwa janga na dharura ya
dunia.
Dr Ben
Newman mtafiti wa masuala ya virusi katika chuo kikuu cha Reading
anasema kuitangaza Ebola kama dharura ya dunia itasaidia
"Kama
itakubalika hali hii kutangazwa kama suala la dharura itawaruhusu
kuingia nchini na itawaruhusu kutoa msaada. Msaada kwa maana ya watu,
usalama wa madaktari, na itawaruhusu kutoa misaada ya kifedha. Hiyo ni
muhimu kwa sababu miundo mbinu katika baadhi ya maeneo yenye virusi
haitoshi" amesema Dr Newmana.
Mbali
na kutangaza ebola kuwa hali ya dharura pia shirika hilo la Afya duniani
limesema kuwa mapema wiki ijayo litakuwa na mkutano wa wataalamu wa
maadili ya afya kujadili uwezekano wa kutumia matibabu ya majaribio ili
kudhibiti Ebola.
Tamko
hilo linakuja kufuatia wamarekani wawili walioathirika na Ebola kupewa
dawa hiyo 'Zmapp' na kuonekana kupata nafuu. Dr Derek Gatherer mkufunzi
katika chuo kikuu cha Lancaster amesema maamuzi juu ya matumizi ya dawa
ya majaribio huenda yakawa magumu.CHANZO BBC SWAHILI
0 Comments