Flora Mbasha akiwa na mumewe Emanuel Mbasha wakati wa furaha ya ndoa yao
ZIKIWA zimepita siku chache toka
kumalizika kwa sakata la mume wa Flora Mbasha kutuhumiwa kumbaka
shemeji yake na Flora Mbasha kuhusishwa katika mchezo huo ,baadhi ya
wadau wa mwimbaji huyo mkoani Iringa wamempa ushauri wa bure mwimbaji
huyo kuwa kwa sasa ni vema akakaa kando na uimbaji wa nyimbo za injili
na badala yake kujikita na uimbaji wa muziki wa bongo Flever
Wakizungumza mtandao huu wadau hao
Hosea Kalinga na Neema John walisema kuwa heshima kubwa ambayo
msanii huyo alikuwa ameipata imeporomoka kwa kasi kubwa kufuatia
matukio mabaya yaliyoikumba familia yake na hivyo hata kama
waandaaji wa matamasha ya injili watamwalika mwimbaji huyo ni wazi
wanaweza kuambulia patupu kutokana na kupotea ghafla katika mionyo ya
watu .
"Tulikuwa tukimkubali sana Flora
Mbasha na Mumewe enzi wakiimba pamoja ila kwa matukio haya ya kidunia
ambayo yamewakuta hakuna mpenzi wa nyimbo za injili atakayempenda
mwimbaji huyo na nyimbo zake ni vema akatafuta soko la uimbaji katika
miziki ya dunia kama bongo Flever na sio injili tena"
Kuanza kubezwa kwa mwimbaji huyo
kumekuja kufuatia mgogolo wa ndoa yake ulioibuka kutokana na sakata la
mume wake kudaiwa kumbaka shemeji yake huyo Flora Mbasha akidaiwa
kuwa na mahusiano na mmoja kati ya wahubiri wakubwa hapa nchini . |
0 Comments