Uonevu! Rapa
mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa
kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake
na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani
kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa
huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa
kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani
kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba
Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi
mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.
CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa
kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba
alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda
huo alikuwa nyumbani kwa Ray C Changanyikeni.
UNGA WATAJWA
Sosi
wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama
na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C,
wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili
kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo
ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.
CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi
kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani
wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid
Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko
walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.
KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.
RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada
ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa
majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani
waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika
Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na
kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio
kwa kipigo kikali walichopokea.
RAY C AVUJA DAMU
“Ray C
aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa
akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine
baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine
kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz
kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.
RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia
na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia
mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.
“Alinipiga
vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo ambalo
lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu hadi kuja
kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye nilitoka naye
ofisini kwangu.
“Ujue
jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na Mariam,
sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo
nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.
“Huko
nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada ya
kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za
kuondoa sumu.
“Tumeendelea
kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna baadhi ya kazi
nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu. Pia alishawahi
kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa alikataa na
kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai mimi ndiyo
namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.
“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”
SOO LIPO POLISI
Ray C
alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi
cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz
anasakwa na polisi.
Juhudi
za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani
hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi anaweza
kutupigia.
CHID BENZ NI TATIZO?
Chid
Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati
akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo,
Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye
Mwanaisha.
Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.CRDT GPL
0 Comments