Makamu
wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokewa na Meneja
Mahusiano wa Benki ya NBC Tanzania, William Kallaghe na Mwenyekiti wa
Bodi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) alipoalikwa kama mgeni rasmi katika
hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar
es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita katika Hoteli ya Serena.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (wa pili kushoto) Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale (kushoto),
wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakijumuika pamoja katika hafla ya
futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu ( kushoto) akiwaongoza
baadhi ya wateja wa benki hiyo kushiriki futari waliyowaandalia jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya
NBC ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa
karibu wateja wao.
0 Comments