WINDHOEK,
NAMIBIA JULY 7, 2014: Familia ya Cheka ni moto wa kuotea mbali baada ya
kuendeleza ubabe wao katika masumbwi baada ya Cosmas Cheka ambaye ni
mdogo wake bingwa wa zamani wa IBF/Africa Super Middleweight, Francis
Cheka kumwadhibu bila huruma bingwa wa dunia wa vijana wa IBF Albinus
Felesianu wa Namibia na kutoka naye sare nyumbani kwake Windhoek,
Namibia.
Hata hivyo, matokeo hayo yalipingwa na mashabiki wengi nchini Namibia na kusema kwamba ushindi ulikuwa wa wazi kwa Cosmas Cheka
Mpambano
huo uliohudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa ngumi toka nchi za Kusini
mwa Africa ulifanyika katika ukumbi wa hoteli ya nyota tano ya Windhoek
Country Club Resorts & Casino iliyoko katika mji mkuu wa Namibia
Windhoek July 5, 2014.
Cosmas ambaye aliondoka nchini Tanzania mwenyewe bila
msaidizi yeyote na wala hakukuwa na Mtanzania mwingine katika pambano
lake zaidi ya msimamizi mkuu wa mpambano huo na Rais wa IBF barani
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Onesmo Alfred McBride
Ngowi, aliubadilisha ukumbi mzima kuwa wake kwa kushangiliwa na kila mtu
bila kujali walikotoka.
Akipigana kwa kujiamini na kutumia staili ya bondia
bingwa wa dunia wa zamani Mohammed Ali ya kurukaruka kama kipepeo na
kuuma kama nyuki (Fly like a Butterfly, Sting like a Bee.) Cosmas alionyesha kipaji cha hali ya juu cha kuzichapa ngumi.
Aliuanza mpambano kwa kutoka kwenye kona yake ya rangi ya
bluu na kuanza kumiminia ngumi za heshima bondia huyo bingwaa wa dunia
kwa vijana Albinus Felesianu bila huruma na kuanza kushanguliwa mapema
kabisa na mashabiki waliofuatana na Albinus bila kujali taifa
alilotoka. Wengi walisikika wakisema kuwa wanafurahia mchezo wake wa
kuvutia na kuwa hawajawahi kumwona bondia kutoka nje kwenda Namibia na
kufanya alichokifanya Cheka.
Akisadiwa na kocha wa bondia Bongani Mahlangu kutoka
Africa ya Kusini ambaye naye alipigana baada ya pambano la Cosmas na
kupigwa na bingwa wa IBF/Afrika uzito wa Lihht “Energy” Abraham
Ndaendapo wa Namibia, Cosmas alipigana kama mabondia wengi wa nchini
Marekani wanavyopigana.
Mstahiki Meya wa jiji la Windhoek alisimama kumshangilia
Cosmas ilipofika raundi ya nane ambapo aliuamsha ukumbi mzima
kumshangilia bila kujali kama alikuwa anapigana na Mnamibia mwenzao.
Nayo
timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Afrika ya Kusini Banyana Banyana
ambayo iliifunga timu ya taifa ya Namibia mchana huo, ilikuwa inaimba
nyimbo za kivita wakati Cosmas alimwadhibu Albinus Felesianu na
kuufanya ukumbi mzima kuwa sherehe za nguvu.
Jajji wa Namibia Lazarus Nainda alimpa ushindi wa 115
Cosmas na 109 Albinus. Jaji Richard Kabamba - Muya wa Kongo DRC alimpa
Albinua ushindi wa 114 na Cosmas 113 na jaji Neville Hotz wa Afrika ya
Kusini alitoa sare kwa 114 kwa 114 na kufanya pambano hilo kuwa sare.
Majabali hao wawili vijana watarudiana tena baada ya
kipindi cha miezi miwili ili kumpata bingwa kweli wa mkanda wa ubingwa
wa IBF Africa, Middle East & Persian Gulf uzito wa Light.
Kuna
uwezekano mpambano wa marudiano ukafanyika Tanzania au Namibia kutokana
na IBF kutoa nafasi ya kufanyika katika mojawapo ya nchi hizi m
bili.
Mpambano wa ubingwa wa IBF Africa, Middle East &
Persian Gulf uzito wa Light uliandaliwa na kampuni ya Warriors
Promotions ya jijini Windhoek, Namibia na kudhaminiwa na kampuni ya simu
ya Namibia ya Telecom Namibia.
Kamishna mkuu wa mpambano huo alikuwa ni Rais wa IBF
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzanai Onesmo Alfred
McBride Ngowi. Refarii alukwa Herman Gurus-Oab wa Namibia wakati majaji
walikuwa Richard Muya wa Kongo DRC, Neville Hotz wa Afrika ya Kusini na
Lazarus Nainda wa Namibia.
Cheka alipata marafiki wengi sana kiasi kwamba ilibidi
Bodi ya kusimamia ngumi nchini Namibia imwekee ulinzi maalum wa Police
ili kumwondelea adha ya kubughudhiwa na mashabiki wengi ambao walikuwa
ni wanawake.
Tembelea tovuti yetu ujue mambo mengi kuhusu IBF Africa, Middle East & Persian Gulf katika:
0 Comments