Waathirika wa mafuriko Mbeya bado wanahitaji msaada-Margareth Esther Malenga, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya



 




Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (katika) akiongozana na Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu ”Red Cross” Mkoa wa Mbeya, Bw. Ulimboka Mwakilili, wakikagua maeneo yaliyoathirika na Mafuriko wakati walipokwenda kukabidhi msaada wenye thamani ya Shilingi Milion 10 kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (kulia), akipokea msaada wa vyandarua kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu ”Redcross” kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wa wilaya hiyo toka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto), pamoja na Mkuu wa Vodacom Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Bw. Macfyden Minja (katikati). Msaada wa jumla ya shilingi Milioni 10 kwa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (kulia) akipokea msaada wa vyandarua kupitia chama cha Msalaba Mwekundu”Redcross”kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wa wilaya hiyo, toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Bw. Macfyden Minja. Anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule. Jumla ya shilingi Milioni 10, zimetumika kwa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kajunjumele iliyopo wilayani Kyela, iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni, alipotembelea shule hiyo, mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya hiyo (hayupo pichani),kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akiingia kwenye moja ya darasa lililoathirika na mafuriko hivi karibuni katika Shule ya Msingi Kajunjumele, iliyopo Wilaya ya Kyela, alipotembelea shule hiyo, mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya hiyo (hayupo pichani), kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wilayani humo. (Picha zote na mpigapicha wetu)

Post a Comment

0 Comments