Timu
ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania jana April 06 imefanikiwa
kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada kuifunga Burundi
mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro
Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi kwenye mechi hiyo akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0,Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

0 Comments