Mbunge
wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye fulana ya
mistari mbele) akizungumza na baadhi ya kinamama wakazi wa Mji wa
Kigamboni waliojitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni kwa
ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa
Kizazi kwa kina mama inayoendelea kutolewa leo kituoni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akimuuliza
Muuguzi wa zamu namna zoezi hilo la Utoaji wa Huduma ya Uchunguzi na
Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye Kituo cha Afya
Kigamboni.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kigamboni,Dkt. Ansilla Lasway
(kushoto) akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine
Ndugulile namna wanavyoendelea kutoa huduma za matibabu mbali mbali kwa
wananchi wa Kigamboni.Mh. Ndugulile alitembelea kituo hicho leo ili
kuona namna huduma zinavyotolewa kwa wagonjwa na changamoto
zinazokikabili kituo hicho na kuahidi kuzifanyia kazi haraka
iwezekanavyo.
Mbunge
wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwapongeza kinamama
wa Kigamboni kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni
na kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango
wa Kizazi inavyoendelea kwenye kituo hicho.
0 Comments