Na Mwandishi wetu
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa taarifa kwa umma likionya kuhusu vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yenye lengo la kuchochea kuliingiza Jeshi katika mambo ya siasa.
Kanali Bernard Masala Mlunga , ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilibainisha kuwa baadhi ya hoja zinazochochea siasa hutolewa na watu walio katika mazingira ya kijeshi , wale wanaojinasibisha na Jeshi , au waliokuwa wameachishwa Jeshi kutokana na
tabia na mwenendo mbaya, pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.
Kutokana na hali hiyo, JWTZ limewahakikishia Watanzania kwamba linaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chao.

0 Comments