Rogart Hegga 'Katapila' mmoja wa viongozi na waimbaji wa Ruvu Star |
Mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Rogart Hegga 'Katapila' alisema nyimbo hizo zimetungwa na waimbaji watatu tofauti ukiwamo unaitwa 'Kioo' ambao ni utunzi wa kiongozi mkuu wao, Khamis Kayumbu 'Amigolas'.
Alizitaja nyimbo mbili za mwisho kuwa ni 'Chewa Original' wa Seleman Muhumba na 'Facebook' wa Mkuu wa Jukwaa, Victor Mkambi ambaye pia ni mpapasa kinanda mahiri nchini.
"Tunamalizia nyimbo zetu tatu za mwisho kukamilisha albamu kabla ya kuanza maandalizi ya uzinduzi wa bendi na albamu hiyo, pia tumesaini mkataba na kampuni ya kurekodi video ya albamu hiyo."
Aliongeza, video hiyo inatarajiwa kuanza kurekodiwa wiki ijayo kwa nyimbo tatu za awali ambazo ni; 'Spirit' alioutunga yeye (Hegga), 'Network ya Mapenzi' wa Toto Tundu na 'Jua Kali' wa Kuziwa Kalala.
"Video hiyo itaanza na nyimbo za awali tulizotambulisha kwa mashabiki na tukimalizia hizi tunazorekodi tutahimisha albamu na ndipo mipango ya uzinduzi," alisema.
Alisema bendi yao ipo hatua ya mwisho kabla ya kuanika ratiba ya maonyesho yao kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka itakayoptangazwa muda wowote kuanzia leo ili mashabiki wao wakae tayari kuwapokea.
0 Comments