Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
inaendelea kesho (Aprili 12 mwaka huu) katika raundi ya 25 ambapo Simba
na Ashanti United zitapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10 kamili jioni.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Rhino Rangers (Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union itakuwa
mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Keshokutwa
(Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi nyingine nne za kukamilisha
raundi hiyo. Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa
Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo
Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
0 Comments