SIMBA YASHIKA NAFASI YA TATU BAADA YA KUTOKA SARE NA MTIBWA



Simba leo imetoka sare na Mtibwa ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mtibwa ndio walianza kuliona lango la Simba kupitia kwa Musa Mgosi na Simba kuzawazisha kupitia kwa Amis Tambwe.
Kwa matokeo hayo Azam wanaendelea kuongoza ligi huku Yanga wakiwa nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31 sawa na Mbeya City ila simba inaizidi kwa mabao ya kufungwa na kufunga
Kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya Tanzania Prisons na Coastal Union hazikufungana 0-0

Kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting nao wamelala 0-0
Chamazi, Dar es Salaam JKT Ruvu imefungwa na Ashanti United bao 1-0 na Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Rhino Rangers vs Oljoro JKT zimetoka sare 2-2

Post a Comment

0 Comments