TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA KIBADA,KIGAMBONI, DAR



 Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane
 Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akipokea ufunguo kutoka kwa Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) tayari kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati hiyo, Nassoro Sande (kulia) na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo.
 Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
 Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane  akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Diana Salvatory baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.

 Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Hidaya Mshindo baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji cha msaada katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.
 Wakifurahi baada ya kuzindua kisima hicho

 Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ipopo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwasidia kisima hicho, hivyo kupunguza kwa asilimia kubwa tatizo la maji katika zahanati hiyo.
 Mkazi wa Kijiji cha Kibada akitoa shukrani wa TBL kwa msaada huo.
 Wakazi wa Kibada wakiangalia kisima hicho
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi ya maji nchini ambapo kwa mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil. 450 kwa kazi hiyo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Post a Comment

0 Comments