TAMASHA LA AFTER SKUL BUSH LAFANA NDANI YA MBALAMWEZI BEACH



 Mashabiki kibao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwaani jioni ya leo. 
 Baadhi ya wasanii chipukizi kutoka anga ya muziki wa Bongofleva pia walipewa nafasi ya kuonesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa vilivyo.
 Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.
 Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji
 DJ Mahiri kutoka Clouds FM akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali jioni ya leo.
 Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar. 
 Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM,Hamis Mandi a.k.a B Dozen akitoa utaratibu mzima wa tamasha hilo utakavyofanyika.Tamasha hilo limeratibiwa na Clouds FM kwa kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd.
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
Mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakifuatilia kwa makini

Post a Comment

0 Comments