Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia zawadi ya Krismas na Mwaka Mpya
Binti Asnah Sudi, kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Umra
kilichoko Magomeni, wakati wa sherehe ya mwaka kwa watoto yatima
aliyoiandaa kwa kushirikiana na Twiga Cement na Klabu ya Rotary ya Dar
es Salaam tarehe 14.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia baadhi ya michezo iliyokuwa
ikichezwa na watoto yatima kutoka baadhi ya vituo hapa Dar es Salaam
kwenye sherehe ya mwaka ya watoto hao iliyofanyika tarehe14.12.2013.
Father
Krismas akiwagawia watoto yatima zawadi zao wakati wa hafla
iliyoandaliwa na Mama Salma Kikwete kwenye ofisi za WAMA, tarehe
14.12.2013.
Baadhi
ya watoto yatima kutoka vituo vya kulelea vya, Umra, Kurasini MUMalaika
wakiwa katika hafla ya kumaliza mwaka zilizofanyika kwenye ofisi za
WAMA. Sherehe hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Twiga Cement, Rotary Club
na WAMA tarehe 14.12.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI
0 Comments