SHUGHULI YA MAZISHI YA MZEE NELSON MANDELA ZINAZOENDELEA KIJIJINI KWAKE QUNU



Kamera ya Globu ya Jamii ipo Ndani ya Hema maalumu ambamo shughuli ya mazishi ya marehemu Nelson Mandela inaendelea hivi sasa katika kijijini Qunu.na kama ilivyo ada ya libeneke la Globu hili kwamba halilali na litakuwa linakuletea Live matukio yote yanayoendelea katika Mazishi ya Shujaa huyo wa Afrika na Dunia kwa Ujumla
 Rais Jakaya Kikwete ni mmoja wa viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye mazishi ya hayati Mzee Nelson Mandela yanayofanyika leo kijijini kwao Qunu, nchini Afrika Kusini.
Watu wengi maaruru Duniani wapo eneo hili hivi sasa kuhudhulia mazishi ya Mazishi ya Mzee Nelson Mandela yanayoendelea hivi sasa katika kijiji cha Qunu,baadhi yao ni Oprah Wilfrey,Forest Whitaker,Richard Branson,Idris Ebra na wengine wengi.
Mwili wa Mzee Mandela ukiwasili ukumbini.
Rais wa Zamani wa Zambia,Mzee Keneth Kaunda pia yupo.

Post a Comment

0 Comments