P –SQUARE WATETA NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, WATEMBELEA NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO WALEMAVU DAR



Wanamuziki kutoka Nigeria, Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
  Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
 .Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea  mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi  na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.

Post a Comment

0 Comments