BINGWA wa taifa wa ngumi za kulipwa nchini, Japhet Kaseba usiku wa kuamkia leo amekumbana na kipigo cha KO ya raundi ya pili toka kwa mwenyeji wake, Jeremy van Diemen katika pambano la kimataifa la uzito wa Light Heavy lililochezwa nchini Australia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa, Mtanzania hatua huyo hakuweza kuhimili makali ya mpinzani wake na kukubali kipigo cha KO ya raundi ya pili tu ya mchezo huo uliokuwa uwe wa raundi sita uliochezwa kwenye ukumbi wa Metro City.
Inaelezwa Kaseba anayefahamika kama Champion, alionyesha upinzani katika raundi ya kwanza tu, kabla ya kushindwa kuhimili ngumi nzito za mpinzani wake ambaye katika mapambano saba aliyocheza sasa ameshinda matano manne kati ya hayo ni ya KO).
Kabla ya Kaseba kudundwa, bondia mtanzania mwingine,m Jonas Segu naye alikumbana na kipigo kama hicho cha KO baada ya kunyukwa na Luke Sharp katika pambano la utangulizi uzito wa kati.
Segu alishindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 5 raundi moja kabla ya kuhitimisha pambano hilo na kuendeleza unyonge wa mabondia wa Tanzania wanapoenda kucheza nje ya nchi kwa kupigwa kila mara.
Mabondia hao wawili wanatarajiwa kurejea nchini kesho kinyonge.
0 Comments