RAGE AZOMEWA UWANJANI TABORA



Na Mwandishi Wetu., Tabora

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage,jana alijikuta kwenye

wakati gumu kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kukumbwa na

nyimbo zilizomkejeli huku kukiwa na zomeazomea ya chinichini toka kwa

kikundi cha hamasa maarufu kama ‘Wakali na Mnarani’.

 

Rage alikumbwa na zomea zomea na nyimbo za kejeli mbele ya mkuu wa

mkoa wa Fatma Mwassa,mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Suleiman

Kumchaya,wakati timu ya Simba SC ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya

Rhino Rangers ya Tabora.

 

Hatua nyimbo hizoo kuanza kuimbwa ilianza pale timu ya Rhino Rangers

kupata goli kwenye dakika ya 15 ndipo kundi hilo lilipoanza kuimba

nyimbo za kejeli dhidi ya Rage huku wakimtaja kwa jina lake kwa nguvu.

 

Nyimbo ambazo kundi hilo ambalo nalo linafanana na kundi maarufu la

Muchacho la jijini Dar-es-Salaam,waliaanza kuimba ‘mbunge  wetu timu

mbovu aibu kwako’, ’mbunge wetu ingia ucheze’.

 

Aidha nyimbo hizo za kutunga papohapo nyingine zilisikika hivi ‘mbunge

timu mbovu ingia ucheze wewe’ ‘kama hali ndo hii 2015 itakuwaje’,huku

wakidai tuachie Simba yetu ubaki na ubunge wako,….na mara nyingine

walisikika wakitamka kila jambo hawezi aaaa!

 

Wakati hayo yakiendelea mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa na mkuu wa

wilaya ya Tabora mjini Suleiman Kumchaya waliokuwa wakiingia uwanjani

kwa nyakati tofauti,Mwassa aliimbiwa mamaa mamaa huyo…mamaa.huku

Kumchaya akiimbiwa baba baba baba karibu.

 

Aidha vijana hao ambao muda wote walikuwa wakiimba nyimbo za kumkejeli

Rage walikuwa hawachoki kiasi mara kadhaa watazamaji waliacha

kuangalia mpira na kuanza kuwangalia vijana hao kwa vicheko.

 
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge Rage kujikuta kwenye hali

hiyo,baada ya mwezi jana mbunge huyo na baaadhi ya viongozi wa CCM

kukumbwa na zomezomea kwenye mkutano wao wa hadhara. 

Hata hivyo wakati vijana hao wakiendelea na nyimbo zao Rage alionekana

kutokuwajali.

 

Katika meechi hiyo timu ya Simba Ilishinda kwa goli 3-1,magoli ya

Simba yakifungwa na Nassor Masoud Chollo goli 1,Edward Christopher

goli mbili na goli la Rhino Rangers lilifungwa na Said Kipanga.
 

 

Post a Comment

0 Comments