Na Elizabeth John
MWANADADA
anayetamba katika tasnia ya muziki wa Taarabu nchini, Salma Swed ‘Salma
Segere’ ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Nyota Njema’
ambao umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Mbali
na kibao hicho mwanadada huyo alishawahi kutamba katika vibao vya
Segere, Lindima, Alongore na vinginevyo ambavyo vimeimbwa na kundi la
muziki huo la Wazazi Culture Troup ‘Segere Original’.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Salma Segere alisema anamshukuru mungu kazi
hiyo inafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo ikiwa ni pamoja na
kupokelewa vizuri na mashabiki wa Taarabu nchini.
“Namshukuru
mungu kazi hii imepokelewa vizuri na mashabiki wangu, kwani tasnia ya
muziki sasa ina wasanii wengi sana hadi kazi yako ikikubalika ujue
umefanya kazi nzuri na umeumiza sana kichwa,” alisema.
0 Comments