SHIRIKISHO la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation)
kwa kushirikiana na Kamati ya
kuratibu mazishi ya marehemu Albert
Mangwea ‘Mgwair’ aliyefariki anchini Afrika Kusini mapema wiki hii akiwa katika shughuli zake
za kimuziki wanawaomba watanzania wote kumchangia ili kufanikisha taratibu zote
za mazishi.
“Tunapenda kuwajulisha
watanzania kuwa kama mambo
yatakwenda kama yalivyopangwa basi mwili
utawasili siku ya Jumamosi jioni Juni mosi.
Mara baada ya kkupatikana kwa taarifa za msiba huo kamati iliundwa ikiwa chini ya Mwenyekiti
ambaye ni kaka wa marehemu Keneth Mangwea.
“Akizungumza kuhusu bajeti ama hesabu kamili inayohitajika
Novemba anasema bado hawajatambua kiasi kamili cha fedha inayohitajika ila
anasisitiza jambo la msingi ni kujitolea katiuka kuichanga fedha ili
kukamilisha msiba huu” anasema Ado.
Wanavyomzungumzia baadhi ya wasanii
Jay Moe anasema kwamba yeye alikuwa akiwasiliana naye mara
kwa mara kabla hata alipokuwa nchini Afrika Kusini.Na pindi alipoulizwa na
mwandishi wa makala hii kama wanamtambua Promota ambaye alimpeleka msanii huyo
bondeni , Jay Moe anakiri kwa kusema kwamba ni promota ambaye amekuwa akifanya
kazi na wasanii wengi hapa nchini.
“Ngwair aliondoka nchini kama wiki tatu zilizopita na shoo zake aliandaliwa na promota mmoja
ambaye ni mtanzania anayeishi Afrika Kusini anaitwa Pizzo.Anaendelea kwa kusema
kuwa unajua tukiwa Afrika Kusini huwa tunakwenda kwa ajili ya shoo moja tu
lakini kwa kuwa kule Watanzania wako wengi na wanaishi katika miji mbalimbali
hivyo huomba shoo nyingi na msanii kujikuta anafanya zaidi ya shoo alizopanga
ndivyo ilivyokuwa kwa Ngwair” anasema Moe.
Anaeleza kwamba Ngwair alifanya shoo katika miji ya
Pretoria, Capetown na Johanesburg ambako ndiko mauti yalimfika.
Moe anasisitiza kwa kusema kuwa Pizzo ni Promota mkubwa
ambaye pia amewahi kuwachukua wasanii kama TID, Mr.Blue na wengine wengi kwenda
kufanya shoo Afrika Kusini.
Kama hiyo haitoshi Rais wa Shirikisho la Muziki nchini Ado
anasisitiza kwa kusema kwamba
haiwezekani kwa wasanii wawili wamalize shoo halafu walewe hadi maafa
yatokee lakizima kuna kitu siyo bure anasisitiza November.
“Jamani Watanzania wenzangu tusichukulie mzaha jambo hili
tulitazame kwa kina hapa lazima kuna
kitu siyo bure na tunahitaji uchunguzi wa kina wa kifo cha Ngwair” anasema November ambaye pia muimbaji wa nyimbo za
Injili na kitaaluma ni Wakili.
November anaongeza kwa kusema kwamba gharama ya kuuleta mwili peke yake kuwa
kunahiutajika kuwe na kiasi cha Dola za Kimarekani 6000 ambazo sawa n ash. Mil.
11 za Kitanzania.
Wakati huohuo anasisitiza kwamba kamati haitapokea fedha
hivyo masuala ya fedha wameyaacha kwa familia ambapo kaka wa marehemu atatumia
MPESA yake kukusanya fedha ambayo ni 0754967738 na Akaunti yake ya NMB
02505841.Pia November anasema kwamba kwa sasa wanapokea misaada ya vitu kama
vile kufungiwa maturubai, chakula, maji, usafiri , viti na mahitaji kadhaa ya
kibidanamu ambapo mtoaji atatakiwa kupiga simu ya Mwenyekiti wa Kamati Adam
Juma0754 074323.
Pia ametoa wito mwingine kwa watanzania kumwombea msanii ‘M
to the P’ili apone haraka ambaye mpaka
sasa bado amelazwa huko Afrika Kusini na
wamchangie kwa hali na mali pia.
Akizungumzia kuhusu wasanii kutumia dawa za kulevya anasema
kwamba jambo hilo kwa sasa liachwe kama lilivyo watalizungumzia baada ya msiba
kupita.
“Suala la wasanii wetu kujihusisha na matumizi ya dawa za
kulevywa kwa kweli linasikitisha lakini kwa leo tuliache tutalizungumzia siku
nyingine kwamza tuache huu msiba upite” anasema November.
Naye Mtayarishaji P Funk ‘Majani’ anasema anaumia sana na
msiba huu huku akisema katika maktaba yao wananyimbo na albamu nyingi
alizofanya na marehemu ambapo atakapotulia atatoa moja baada ya nyingine.
Akizungumzia kuhusu kuzuia Kampuni ya Clouds Media Group
kutotumia nyimbo za Ngwair anasema ni kweli amewazuia wasipige lakini nkwa kuwa
yeye hana nguvu wanaendelea kuzipiga ila anaimani siku moja atafanikiwa na
jamii itaelea maana halisi anayopigania.
Wakati huohuo Majani anaeweka wazi suala la wasanii kujikita
katika matumizi ya dawa za kulevya kwamba zinatokana na kuwa masikini wakutupwa
hivyo kuona kwamba ulevi njia moja wapo ya kumpotezea mawazo.
“Lazima wasanii wawe walevi ni kwa sababu ya kujiona anajina
kubwa lakini hana nyumba hana gari hukui
kazi zake zikizagaa na kunyonywa na wajanja wachache” anasema Majani.
Msiba wa Ngwairt upo Mbezi Beach Goigi jijini Dar es Salaam.
Simanzi imetawala kwa
watanzania na wapenzi wa muziki nchini baada ya kupata taarifa za msiba wa
ghafla wa msanii wa muziki wa kizazi kipyaNgwair.
Ngwair aliyefariki dunia juzi nchini Afrika Kusini, akiwa
usingizi akiwa na Rafiki yake M To The P
ambaye naye hali yake ni mbaya sana.
Profesa Jay amlilia akisema Ngwair niliyeanza kumfahamu
mwaka 2004 katika ziara ya kimuziki ya uzinduzi wa albamu yangu iliyokwenda kwa
jina la Gheto Langu kwa mara ya kwanza
nilimwona Dodoma akiwa katika kundi la East Zoo.
Ngwair alinivutia aliwa ni kati ya kundi la wasanii wa
Dodoma alieanza kuwika kuwika akitokea
katika kundi lililoundwa na Dark Master, Noorah na Mez B.
Ngwair akiwa rafiki mkubwa wa Jumanne Mohamed Mchopanga
maarufu kama Jay Moe waliweza kupanda jukwaa
na kuimba kwa kutumia muziki mtupu na kumfanya awike katika ziara hiyo
maalum.
Mwanamuziki huyo aliporejea Dar es Salaam kutoka katika
mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mara na wanza, Ngwair aliingia hatua nyingine kwa
sababu alizidi kupata uzoefu kwa kuwa
alikuwa na wasanii wengi maarufu ambao aliweza kujua ni kitu gani kimefanya
wafike hapo kimuziki.
Ngwair aliweza kufanya ziara hiyo akiwa amepata nafasi
kutoka kwa waandaji wa zaiara ile ambao ni Kampuni ya Prime Time Promotions.
“Si rahisi kutaja kila kitu lakini kiukweli namkumbuka sana
kwa mchango wake mkubwa aliyoutoa ikiwa ni pamoja nae ukweli utabaki
kwamba alipenda sana kazi yake kwa
kutumia maneno ya mtaani na kuweza kutoa ujumbe mzuri katika nyimbo zake”
anasema
Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza
kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya
muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote,
ikiwemo gari aliyokuwa anaimilikia aina
ya Jeep.
Haikuishia hapo kwani Ngwair alijikuta akitoka kwenye uwezo
wa kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam hadi kuishi
katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou
Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo
yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi
kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya
na ‘kuharibika zaidi’.
Mafanikio ya Ngwair kimuziki
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music
Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
Historia Fupi ya Ngwair
Asili ya Ngwair ni
mkoa wa ruvuma, alizaliwa mkoa wa mbeya Novemba 16 1982 alikua ni mtoto wa
mwisho katika familia yao ambaye alipata elimu yake ya msingi mkoani Dodoma, shule ya msingi Mlimwa na kusoma
Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.Ni mtoto wa mwisho yaani wa 10 kuzaliwa kwa baba huku kwa
mama yake akiwa ni mtoto wa sita.
Enzi za uhai wake aliachia nyimbo nyingi ambazo zimepelekea
umaarufu wake kama: Kama ni demu Sikiliza akiwa na Lady Jay Dee, Mikasi
aliyoifanya chini ya Ludigo na nyingine nyingi zilizokuwa katika album ya Mimi.
makala hii imeandaliwa na bongoweekend.blogspot.com

0 Comments