MHANDISHI WA MAJI NJOMBE AKUTWA AMEKUFA KATIKA KISIMA CHA MAJI



 Kikosi cha Zima moto na uokoaji cha Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na wananchi wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Mgambo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho jana katika Uwanja wa ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
 Mwili wa Eng.Abdalah Mgambo ukionekana kwa umbali kwenye gari la Polisi ukipelekwa hospitali Kibena kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
 Wa pili kushoto ni Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Mji wa Njombe Eng.Abdalah Mgambo enzi za uhai wake wakati wa Kilele cha Wiki ya Maji March 22 mwaka huu katika kijiji cha Igominyi.
Marehemu Abdalah Mgambo enzi za Uhai wake akisoma taarifa ya Hali ya maji katika halmashauri ya Mji wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu wakati wa kilele cha wiki ya Maji Igominyi Njombe.
Taarifa toka eneo la Tukio zinasema kuwa marehemu Abdalah Mgambo alikuwa katika Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe kisha akamuaga mke wake kwamba anatoka nje kujipumzisha kwenye gari lake majira ya Saa Moja jioni jana April 30 akatoweka ghafla na kisha Kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.

Akizungumza na Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com eneo la Tukio mara baada ya kuuokoa mwili wa Mhandisi huyo Afisa mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o amesema kuwa leo asubuhi amepata taarifa toka kwa mke wa marehemu kuwa alitoweka ghafla na mara baada ya kuikuta kadi ya ATM nje ya kisima cha maji ndipo wakachukua jitihada za kuanza kutafuta kwenye kisima hicho kwa kushirikiana na kikosi cha Zima moto na Uokoaji cha Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Bwana Mng'ong'o amesema kuwa majira ya Tisa jioni mei mosi ndipo mwili wa marehemu umeokolewa na kuwahishwa katika Hospitali ya Kibena Njombe.

Post a Comment

0 Comments