Sumaye: Malezi ya walimu yakiwa mema Tanzania itakuwa na kizazi kitakachoiogopa rushwa kama sumu inayonuka




Waziri mkuu mstaafu, Mh. Frederick Sumaye akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wahitimu 1029 wa chuo cha ualimu mjini Singida. Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mmiliki wa chuo cha ualimu Singida, Martin Makuza.
Mkurugenzi mtendaji wa Prime Education Network (PEN) Tanzaia, Martini Mkauza akitoa nasaha zake kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu cha Singida mjini. Kulia ni waziri mkuu mstaafu,Frederick Sumaye.
Waziri mkuu mstaafu, Mh.Frederick Sumaye akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu 1,029 wa chuo cha ualimu Singida.
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha ualimu Singida,wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye (hayupo kwenye picha) wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo hicho.
Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Manguanjuki manispaa ya Singida kikitoa burudani kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.
Mmoja wa waandishi wa habari,Damiano Mkumbo akiwajibika kupata picha safi kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Waziri Mkuu mstaafu Ferderick Sumaye amewataka wahitimu wa vyuo vya ualimu wakatimize wajibu wao wa kufundisha kwa bidii na kuwalea vizuri watoto watakaokabidhiwa ili wawe raia wema wa baadaye.
Akizungumza kwenye mahafali ya sita ya chuo cha ualimu Singida kilichopo Singida mjini Sumaye ametoa changamoto hiyo akisema malezi ya walimu yakiwa mema yatatuzalishia Watanzania wa kesho ambao rushwa kwao itakuwa ni sumu inayonuka na ufisadi hautapata nafasi katika nchi yetu na pia madawa ya kulevya hayataingizwa nchini na maovu yote yatatoweka katika jamii.
Akifafanua zaidi, amesema walimu ndiyo wenye turufu ya kuamua ni Watanzania wa aina gani tunataka kuwatengeneza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu huyo mstaafu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wahitimu hao 1,029 kuwa pamoja na mapungufu mengi yanayojitokeza, lakini serikali inajali sana maslahi ya walimu.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Prime Edecation Network (PEN) Tanzania Martin Makuza, ameyaomba mashirika likiwemo la NSSF, kuangalia uwezekano wa kuanza kuwakopesha wanafunzi wa ualimu kwa madai kwamba wanafunzi hao kwa asilimia kubwa, wana uhakika wa kupata kazi na hivyo kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo.

Post a Comment

0 Comments