Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kulia) akisalimiana na Laila
Adam mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati wa warsha
kuhusu ugonjwa wa malaria kwa Wanafunzi wenye Ulemavu iliyodhaminiwa na
benki hiyo mwishoni mwa wiki. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kulia) akisalimiana na Happy
Tadeo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati wa warsha
kuhusu ugonjwa wa malaria kwa Wanafunzi wenye Ulemavu iliyodhaminiwa na
benki hiyo mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya EXIM imeahidi kuendelea kusaidia kampeni mbali mbali zinazolenga kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo nchini.
Akizungumza
katika warsha kuhusu ugonjwa wa Malaria iliyoandaliwa kwa wanafunzi
wenye ulemavu mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant alisema kuwa japokuwa dunia
imepata mafanikio makubwa katika kutokomeza ugonjwa huo, bado ugonjwa
huo ni tishio hasa kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka
mitano huku akibainisha kuwa watu 660,000 upoteza maisha kila mwaka
kutokana na ugonjwa huo.
Semina
hiyo imefanyika siku chache kabla ya maadhimisho ya Siku ya Malaria
Duniani itakaefanyika tarehe 25, April, 2013 na kaulimbiu ya Wekeza
katika vizazi vijavyo, Shinda Malaria.
Grant
aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kufanya usafi katika makazi
yao ilikupunguza uwezekano wa mbu kuzaliana na kuongezeka huku
akiwasisitizia kutumia vyandarua kabla ya kulala.
“Ugonjwa
wa malaria bado ni tishio hapa Tanzania na duniani kwa ujumla. Mpaka
leo, watu 660 000 duniani upoteza maisha duniani wengi wao wakiwa akina
mama wajawazito pamoja na watoto chini ya miaka mitano,” alisema Grant.
Grant
alisema kuwa benki yake itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya
kujikinga dhidi ya ugonjwa huo na kuzisihi taasisi mbali mbali kusaidia
jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.
Naye
Laila Adams kutoka Shule ya Sekondari ya Jangwani wakati akisoma risala
ya wanafunzi wenye ulemavu alisema kuwa watu wenye ulemavu bado
wanachangamoto mbali mbali zakimaisha.
“Kwa
mfano, licha ya Serikali kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo ya
Elimu ya Msingi (MMEM) na elimu ya sekondari (MMES) inayolenga kutoa
fursa zaidi za elimu, idadi ya watoto wenye mahitaji maalum wanaopata
fursa hizo bado ni ndogo ukilinganisha na vikundi vingine.
“
Kwa mfano wakati kiwango cha wanafunzi wanaoandikishwa katika elimu ya
msingi kikiongezeka hadi asilimia 94 mwaka 2011 kutoka asilimia 78 mwaka
2000, watoto walemavu walieandikishwa kuanza elimu ya msingi ni chini
ya asilimia moja,” alisema.
0 Comments