Social Icons

Friday, October 1, 2010

Unamkumbuka mtu huyu? ni galacha katika kuchora katuni

Jina la Ibra Radi Washokera si geni masikioni mwa watu na wapenda vibonzo (Katuni) ambaye hivi sasa ni Rais wa Shirikisho la Chama Cha Muziki wa Tanzania, ambaye alitamba na katuni za Sunche na Kapeto sambamba na hadithi ya vibonzo hivyo kwa ujumla.Pia wadau mtakumbuka ile hadithi ya Mzee Zumo, Obi na Linda bila kusahau Sani, Pimbi Betina na Zena huyu ndiye mchoraji wa vibonzo vile ambavyo hata leo mtu ukiviona utafurahi. Blog hii ilikutana naye katika viwanja vya Chuo Cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ), Ilala Sharif Shamba.Kaa chonjo kwa habari zaidi ambapo nawaahidi kumhoji mambo mbalimbali licha ya kwamba leo alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwam,ba Oktoba Mosi ni siku ya muziki duniani (International Music Federation) kuku akiwaomba wadau kuiadhimisha kwa jinsi watakavyoweza popote pale walipo.

No comments:

 
 
Blogger Templates