|
Shani Ally wa Benjamin akiwa na mpira |
|
Mchezaji Marysiana Edga akijaribu kumtoka Shani Ally wa Benjamini |
|
Wachezaji
waliovaa nyekundu ni timu ya cluster ya Benjamini na njano ni cluster
ya Kinyerezi kabla ya mchezo ambao Benjamini walishind |
|
Mchezaji Nusrat
Msuya wa Kinyerezi akiwa na mpira wakati wa mchezo wao dhidi ya
Benjamini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Jangwani Wasichana |
|
Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji kabla ya mchezo kuanza |
|
Mchezaji wa Benjamin akijaribu kutuliza mpira wakati wa mchezo dhidi ya Kinyerezi uwanja wa Azania |
MASHINDANO ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)
wilaya ya Ilala yameanza leo kwa michezo ya soka, netbali, kikapu, wavu
na riadha kufanyika kwenye viwanja vya sekondari za Azania, Jangwani na
Zanaki.
Kwenye viwanja vya Azania walianza kwa kufukuza upepo ambapo wasichana
na wanavulana walikimbia kwenye mbio za mita 100, 200 na 800 na
washindi kupatikana.
Baadae ulifika wasaa wa soka ambapo timu za Beenjamin walicheza na
Kinyerezi na mpaka Lenzi ya Michezo inatoka uwanjani hapo Kinyerezi
ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 huku Cluster ya Upanga na Ilala wao wakiwa
bado hawajafungana.
Kwa upande wa netbal Benjamini iliifunga Kinyerezi.
Awali akifungua mashindano hayo Mwenyekiti wa Umuja wa Wakuu wa shule za
Sekondari za Ilala aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu kwenye michezo
kwani kama utashindwa darasani michezo inaweza kukuajiri.
0 Comments