SHIRIKISHO
la michezo kwa wizara, idara ,taasisi na mashirika ya serikali limewataka
viongozi wa michezo kudhibitisha mapema ushiriki wao katika mashindano kabla ya
AUGASTI mwaka huu na kutuma majina ya michezo watakayoshiriki.
Katibu mkuu
wa SHIMIWI RAMADHANI SULULU amesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika
SEPTEMBER mwaka huu mkoani DODOMA lakini yamekuwa yakigubikwa na mamluki jambo
ambalo halikubaliki katika mashindano hayo
SULULU
amesema shiriki wanatakiwa kuanza mazoezi mapema ,lakini kulipa ada ya
uwanachama shilingi laki sita, ada ya ushiriki laki nne na mchango wa ujenzi wa
kiwanja laki mbili.
Mchezo
inayoshindaniwa ni soka, netiboli kukimbia, kuvuta kamba, darts, drafti,
baiskeli, karata pamoja na mchezo wa bao.
0 Comments