Na Abdulaziz,Ruangwa
Wachimbaji wadogowadogo wa madini
Wilayani Ruangwa pichani (kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo) wametakiwa kuacha kufanya kazi katika mfumo usio rasmi
badala yake wabadilike kwa kuingia katika mfumo rasmi ambao
utawawezesha kukubalika na taasisi za fedha kutokana na kukua kwa sekta ya
Madini Duniani ikiendana na Mabadiliko ya Uchumi hapa Nchini.
Wito huo Umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya
ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini katika
wilayani humo ambapo alibainisha kuwa uchimbaji mdogo ni sekta ya
kibiashara ambayo inaweza kuongeza kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira
pamoja na uchangia ukuaji wa pato la taifa Licha ya kutokuwepo kwa
taarifa sahihi za uzalishaji na uuzaji wa madini na wachimbaji wadogo
kutozifanya shughuli za uchimbaji madini kama shughuli maalum
ambazo zinaweza kuajiri na kuajiri
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewezeshwa na
Wizara ya Nishati na Madini na kuratibiwa na ofisi ya Kamishna wa
Madini kanda ya kusini na kuhusisisha Wachimbaji
wadogo,Madiwani,Watendaji wa vijiji/kata ambapo mada mbali mbali zitatolewa zikiwamao za
Sheria ya madini ya mwaka 2010,Ufafanuzi wa sera ya madini,Fursa
za madini zilizopo Ruangwa na Matumizi salama ya Baruti ambapo pia
watapewa Mwongozo wa kuandaa mpango wa kutunza Mazingira(EPP0).
|
0 Comments