Katika suala hilo la Kimahakama, Mwesigwa aliishitaki Klabu ya Yanga akiidai kiasi cha Sh. 183,400,050, huku Sendeu akidai kiasi cah Sh. 79, 900,050, ambapo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, aliwahoji wanachama, juu ya hilo na kupata jibu la pamoja kutoka kwa wanachama waliosema kwa pamoja kuwa, ''Wavuliwe uanachama kwa kukosa uzalendo na Klabu yao''.
Ndipo Manji alichukua jukumu la kutangaza kuvuliwa uanachama kwa watu hao na kusema kuwa wamewaongeza wajumbe wawili kwenye bodi ya Udhamini ya Klabu hiyo, ili kutimiza idadi ya watu saba, ambao ni Amir Kungwe na George Mkuchika.
Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV, aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi baada ya timu hiyo ya Yanga jana yake kuonyesha makucha yake na vitu adimu ilivyorejea navyo kutokea nchini Uturuki kwa kuifunga timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans, Yusuf Manji akifafanua baadhi ya mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo, maendeleo ya Klabu hiyo pamoja na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar, Sahihisho la katiba yao, masuala mbalimbali yanayohusiana na wanachama wao, ustawi wa wanachama wao, mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mengi yaliyoongelewa.
Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Beki mahiri wa Yanga, Shadrack Nsajigwa (kulia) akipeana mkono wa shukrani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa, na kuwa mchezaji mwenye nidhamu zaidi, hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement Sanga wakifatilia jambo kwa makini ukumbini humo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
Baadhi ya Wazee wa baraza wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo mkuu wa Kihistoria.
Kocha mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.
Baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo.
Msanii mahiri wa kizazi kipya, Barnaba, pamoja na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke, akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.
0 Comments