Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na
Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika
(OAU),Dr. Salim Ahmed Salim ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Katiba, mara baada ya Mh. Lowassa kutoa maonai yake mbele ya tume hiyo.
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba
mpya,mara baada ya kutoa maoni yake.
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipongezwa na
Mjumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya,Dk. Senkondo Mvungi
mara baada ya kutoa Maoni yake.
YAFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASAA:
Kwanza
ningependa kukupongeza wewe mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume
nzima kwa imani kubwa ambayo Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu
hilo zito na muhimu kwa nchi yetu.
Wananchi
pia wamekuwa na imani kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa tume
hii. Kutokana na hilo wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine hayahusiani
na katiba, yaani siyo ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa miongoni
mwao, kwa hiyo naomba radhi mapema, iwapo maoni yangu haya mengine ,
yataonekana si ya kikatiba.
Katiba yetu
ya sasa ni nzuri, imetuongoza katika umoja na mshikamano wa kitaifa kwa
muda wote huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni vyema
kuwepo na katiba mpya ili kuendana na hali halisi.
Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.
1.ELIMU BURE
Moja ya
haki za mtoto ni kupata elimu. Ningependa suala la elimu bure ya
sekondari liwemo kwenye katiba yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya
sekondari ni bure.Nchi yetu bado ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni
masikini.
Uwezo wao
wa kipato ni mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali inaweza
kugharimia elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya kujenga
taifa lijalo lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata elimu ya
sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.
Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa
watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo,
kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.
2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT
Katiba ya
sasa haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya
uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya
mwaka 1977 inatamka kiujumla tu kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI
WAKE KULINDWA.
Lakini ,
haki hiyo inanyang'anywa na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni za
adhabu sura ya 16(penal code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya
kifo(death penalty or capital punishment) kwa kosa la mauaji ya
kukusudia.
Adhabu hiyo
hiyo pia utolewa kwa kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni
kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA
NA ADHABU YA KIFO HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.
3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI
Katika
sehemu nyingi hapa nchini mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni
kiasi gani cha fedha ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika
kampeni.Iainishe ni matumizi gani ya lazima ambayo mgombea hawezi
kukwepa kutumia fedha katika kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura
kwenda kupiga kura gharama hizo nani azibebe.
Katiba
ifafanue rushwa ni nini kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa
PROPORTIONAL REPRESENTATION ,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi
kuwania majimbo na siyo wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama
chake kupata kura nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii
itasaidia kuondoa kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze
kuwania uongozi.
4.ARDHI
Kwa
mwanadamu, kunyang'anywa haki ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni
sawa na kunyanng'anywa haki ya uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa
nguvu wakulima katika suala la ardhi, na kuwasahau wafugaji.
Wafugaji
wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta
malisho ya mifugo yao, ile ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka
kutafuta malisho huku nyuma imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima
au wawekezaji, hili kwakweli si jambo jema .
Tumeshuhudia
migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi
ningependa katiba hii mpya impe mfugaji haki katika suala la ardhi
kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe, ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe
na hali ya 50,50 situation kati ya mfugaji na mkulima katika suala zima
la umiliki wa ardhi,kikatiba!
0 Comments