WASHINDI WA VING'AMUZI VYA ZUKU NA MAJIRA HAWA HAPA



Safu ya viongozi wa gazeti la majira na washindi wa Shindano la Shinda Biashara na Mtaji
  (Picha na Prona Mumwi).
Zawadi ya Ving'amuzi ikitolewa kwa mshindi wa Kwanza wa Shinda Biashara na Mtaji kupitia ZUKU .
Mshindi wa kwanza wa Ving'amuzi kumi vya ZUKU, William Kahale (wa pili Kushoto) akipokea zawadi yake

 Washindi wa Ving'amuzi vya Zuku na Majira hawa hapa

Na Peter Mwenda
GAZETI la Majira kushirikiana na Kampuni ya ZUKU tawi la Tanzania wametoa zawadi ya ving'amuzi kwa washindi watatu wa Shinda Biashara na Mtaji.

Akikabidhi zawadi hizo, Mhariri Mtendaji wa Majira, Imma Mbuguni alisema shindano hilo ni endelevu na kuwataka wasomaji wa gazeti hilo kuchangamikia nafasi hiyo.

Katika sherehe hizo, mshindi wa kwanza, William Kahale ambaye alipata ving'amuzi kumi na madishi kumi alisema hakutegemea kupata zawadi hiyo kwani hakuamini siku moja atapata nafasi ya kuwa mshindi.

Mshindi wa pili,Emmanuel Magabe aliyezawadiwa seti tano za ving'amuzi na madishi matano alisema atalitangaza gazeti la majira kila anapokwenda kwani ameamini hakuna ujanja ujanja katika kumpata mshindi halali.Mshindi wa tatu Muhaji Hassan kutoka Zanzibar hakufika.

Mkuu wa kitengo cha Usambazaji wa Majira, Sophia Mshangama aliwataka washindi hao watumie nafasi zao kulitangaza gazeti la majira mikoani ili kuongeza marafiki wengine hasa wanawake ambao hawakujitokeza kushindana.

"Tunaomba mkawashawishi wanawake huko mikoani wajitokeze kushindania zawadi za ZUKU kwani tunaamini kuwa Ukimwelimisha Mwanamke mmoja utakuwa umeelimisha taifa zima" alisema Mshangama.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Levi Electonics, Hatevele Mposo ambao ni wakala wa ZUKU alisema zawadi hizo na nyingine zitaendelea kutolewa kwa watanzania ili wapate nafasi ya kutumia chaneli zaidi ya 70
zilizoko ZUKU.

Post a Comment

0 Comments