Afisa Utawala BSL Ibrahim Juma Mohammed amesema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa michango mbalimbali ambayo wamekua wakitoa huku akisisitiza kuwa kwa niaba ya uongozi amechukua maombi yaliyotolewa na kuahidi atayafikisha kwa uongozi wa juu kwa utekelezaji.
Kiwanda Cha Sukari Bagamoyo Sugar (BSL) kilichopo
Wilayani hapa leo Januari 13 2025 wametoa vifaa vya Usalama barabarani ambavyo vitatumika katika kuongoza na kupunguza ajali za barabarani kwa wanafunzi na raia katika Kata ya Zinga.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Afisa Utawala BSL Ibrahim Juma. Mohammed amesema kuwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja viakisi mwanga 80 pamoja na vibao vya kuongoza magari kwenda na kusimama ikiwa ni katika kupunguza ajali za barabarani ambazo imeelezwa kukithiri katika eneo hiyo.
Mohammed amesema kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya kurudisha ikhsani kwa jamii kutoka BSL.
Sgt.Otilia Ponera ametoa elimu kwa kata tisa ikiwamo boda boda na wananchi umuhimu wa elimu ya usalama barabarani ikiwa lengo ni kupunguza matukio ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Zinga A/ Insp. Mwajuma Msofe amesema kuwa
Kata tisa boda boda na wananchi wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ikiwa lengo na lengo la kupunguza matukio ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.
"Tunaushkuru uongozi wa BSL kwa msaada mliotoa leo hii lakoni pia tunaomba mtusaidie pikipiki tano ambazo zitawasaidia Polisi Kata katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa jamii" A/Insp. Msofe amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga ameomba uongozi wa BSL kujenga vibanda na stendi za abiria ili waweze kutumia wakati wa kusubiri usafiri nakujikinga na hali za mvua na jua.
"Tunawashukuru sana BSL kwa msaada huu kwa sababu katika eneo hilo la Kata ya Zinga inatumiwa na wanafunzi zaidi ya 1,000 huvuka kila siku hivyo nawasisitiza wanafunzi,waalimu na raia wengine mzingatie kusimamia alama za usalama barabarani ili kuepuka vifo vya ajali za barabarani" amesema Ndemanga.
"Tunawaomba BSL mtujengee matuta na ikibidi daraja ili raia wanafunzi wawe wanavuka kwa kupita juu huku magari yaendelee kupita chini kama ilivyojengwa daraja la buguruni" amesema DC Ndemanga.
0 Comments