* Asema kuwapa uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi Bucha Fisi
NA BASHIR NKOROMO, GEITA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Katoro Mazemule na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni
16.5 za Halmashauri ya kijiji hicho wafikishwe mahakamani haraka.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara leo, katika mji mdogo wa Katoro, mkoani
Geita, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, ni lazima
wahusika wote wa wizi wa fedha hizo wafikishwe mahakamani kwa kuwa ni
jasho la wananchi.
Fedha
hizo zinadaiwa kuliwa na Mwenyekiti huyo kwa tiketi ya Chadema, katika
kipindi cha mwaka 2010 na 2011 hali ambayo imezusha tafrani miongoni mwa
wananchi na uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho hadi sasa.
Nape
alisema, ni lazima Mwenyekiti huyo na waliohusika wote wafikishwe
mahakamani kwa kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu wa fedha hizo
ilishamaliza kazi yake na ripoti kukabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.
"Kamati
ya kuchunguza wizi wa fedha hizi ambazo ni mali ya wananchi ilishafanya
kazi yake na kukabidhi ripoti kwa mamlaka zinazohusika, sasa
kinachosubiriwa ni nini wahusika hawa kupelekwa mahakamani?", Nape
alihoji na kuongeza;
"Sasa
CCM kwa kuwa ndicho chama tawala, tunaagiza hatua za kuwapeleka
mahakamani wahusika wote zichukuliwe haraka ili haki itendeke".
Nape
alisema, kutotokea kwa wizi wa fedha hizo chini ya uongozi wa
Halmashauri ya Kijiji hicho ambao upo chini ya chama hicho, ni dalili
kwamba kujidai kwao kuwa wasafi na wapigania haki za wanyonge ni sawa na
kilio cha mamba.
"
Kila mara tumekuwa tukiwaambia acheni kuhadaiwa na Chadema, hawa siyo
chama cha siasa ni kundi la wajanja fulani, sasa Wana Katoro mmejionea
wenyewe, mmewajaribu mkawapa halmashauri yenu, fedha wamezitafuna sasa
mnahangaika", alisema na kuongeza;
"Kwa
kuwa mmepata funzo hili, bila shaka hamtaruidia tena, kwani
mmeshafahamu kwamba kuikabidhi uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi
fisi bucha".
Mapema,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, alisema kwenye mkutano
huo kwamba, kama hatua za kuwafikisha mahakamani wahusika
hazitachukuliwa haraka, ataongoza wananchi wa Katoro kuandamana ili
kuhakikisha hatua hizo zinachukuliwa.
Kabla
ya mkutano huo, NMape alifungua shina la wajasiriamali la CCM,
Bugayambele lenye wanachama 53 ambao hushughulika na kazi za kutengeza
fenicha mbalimbali katika karakana yao iliyopo eneo hilo la Katoro.
Akifungua
shina hilo, Nape aliahidi kuwapa sh. milioni moja kwa ajili ya
kuendeleza shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kama
randa za mbao, mashine ya kuchetrza mbao na ujenzi wa banda kwa ajili ya
shughuli hizo.
0 Comments