Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu
Mhamila 'Super D' akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza katika mazoezi ya ngumi ufukwe wa GYKHANA Dar es salaam jana Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
KLABU ya ngumi ya Ashanti Ilala imeota kuwa moja ya klabu
itakayotoa wawakilishi katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka
2016 nchini Brazil.
Klabu hiyo ambayo kwa sasa inaundwa na
chipkizi 18 pamoja na mabondia wakongwe imepania kufanya hivyo huku
ikijitapa kuwa itaanza kufanya maajabu kupitia mashindano ya taifa ya
mchezo huo yatakayofanyika Januari mwakani.
Akizungumza na gaazeti hili Dar es Salaam jana, Kocha wa ngumi wa klabu ya Ashanti pamoja na timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo
Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kwa sasa klabu yake imejikita katika
maandalizi kabambe kuhakikisha inaingiza mabondia wengi katika timu ya
taifa ambao baadaye wataingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi
za kufuzu kucheza Olimpiki.
Alisema tayari jumla ya vijana 18 wanajifua katika Ufukwe wa Gymkhana
Dar es Salaam kwa ajili ya mapambano mbalimbali ikiwemo ya ubingwa wa
taifa ambayo yanaandaliwa na Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT).
Alisema
vijana wengi waliopo kwenye klabu hiyo ni wenye umri chini ya miaka 12
na chini ya miaka 20 ambapo amewataja kuwa umri huo ni mzuri kwani
kijana atakuwa mwepesi wa kuelewa kile ambacho atakuwa anafundishwa na
makocha wake
Super D ambaye anafundisha kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo kwa njia ya DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani.
Super D ametoa wito kwa makampuni
mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio
mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi
0 Comments