Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wananchi wa Mkoa mpya wa Katavi, wakati wa sherehe za
uzinduzi wa mkoa huo mpya zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili
mkoani Katavi jana Nov 25, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi rasmi wa Mkoa mpya wa Katavi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mkoa huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili, mkoani Katavi jana
Nov 25, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Majaribio wa
Kampuni ya CAMARIEC, Eng. Wilson Baitani, kuhusu utengenezaji wa
Mashine ya gharama nafuu ya kukamulia asali, wakati alipokuwa
akitembelea mabanda ya maonyesho katika kilele cha sherehe za uzinduzi
wa mkoa wa Katavi, jana Nov 25, 2012 mkoani Katavi. Wa pili (kushoto) ni
mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Kikombe cha mshindi wa pili katika mashindano rasmi ya
sherehe za uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi, Nahodha wa timu ya Polisi
ya Netiboli mkoa wa Katavi, Lawrensea Sanga, wakati wa sherehe hizo za
uzinduzi zilizofikia kilele jana Nov 25, 2012 katika Uwanja wa
Kashaulili, mkoani Katavi.
Makamu
wa Rais, Dkt. Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakizungumza na
Mbunge wa Mpanda, Zalafi, kupitia CUF, wakati Makamu akiondoka katika
Uwanja wa Kashaulili baada ya kuwahutubia wananchi, jana.
Mwanamuziki
Hamza Kalala na kundi lake la Wanakasimbagu, wakitoa burudani wakati wa
sherehe za uzinduzi huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kashaulili
mkoani Katavi, jana.
0 Comments