Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego akizungumza jambo wakati akifunga jukwaa la sanaa, Kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira , Haji Janabi.
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema inatambua kwamba
Sanaa ni ajira rasmi licha ya kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali za kiuratibu, uongozi na kupewa kipaumbele katika mipango ya
kimaendeleo na Serikali.
Akiwasilisha mada ya Umuhimu wa
Tasnia ya Sanaa katika kukuza Ajira nchini, katika Jukwaa la Sanaa,
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira, bwana Haji Janabi
amesema sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza upatikanaji wa
nafasi za ajira na kipato.
“Kwa Tanzania iwapo tutatumia
vyema uwepo wa ubunifu muafaka katika sekta ya sanaa zetu bila shaka tasnia
hii inaweza kuchangia sana upatikanaji wa nafasi za ajira na hivyo kuchangia
kwa kiasi kikubwa katika kuondoa tatizo la ajira hapa nchini,” alisema
Janabi.
Janabi amesema kwamba pamoja na
hivyo kuna changamoyo kubwa ya kiuratibu na kimuundo ikiwa ni pamoja na
Serikali kutotoa kipaumbe katika masuala yanayohusu sanaa na wasanii pamoja
na mgongano wa kimamlaka kati ya vyombo vinavyohusika na uratibu wa masuala
ya sanaa.
Aidha amesema pamoja na nafasi
nzuri ya kukuza ajira, ujio wa teknolojia umeanza kubana soko la ajira ya
sanaa ambapo kwa sasa teknolojia inapunguza uhitaji wa watu katika ufanyikaji
wa sanaa kwa akitolea mfano katika muziki ambapo vitu vingi vinafanywa na mtu
mmoja hivyo kupunguza nafasi za watu wengine.
Pia amesema ili sekata hii iweze
kuwa ajira nzuri zaidi ni muhimu kukaandaliwa viwango na vigezo kama ilivyo
kwa fani zingine ili kuwe na maradaja ya wafanyaji kazi kulingana na viwango
vya umahiri na taaluma.
|
0 Comments