KHADIJA KALILI KUTOA SOMO KATIKA KONGAMANO BASATA



Na Mwandishi Malum , BASATA
MWANDISHI mwandamizi wa habari za Burudani na michezo wa gazeti la Tanzania Daima  Khadija Kalili pichani kulia ambaye pia ndiye Mwendeshaji wa Blogu ya www.Bongoweekend  amechaguliwa kuwa miongoni mwa wanahabari ambao watatoa mada katika kongamano la wadau litakalojadili juu ya hali nini kifanyike kushuhudiwa kwa mmomoyoko wa maadili katika sekta ya sanaa katika siku za hivi karibuni na hatua gani zichukuliwe ili kukabiliana na hali hiyolililoandaliwa na  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa BASATA  Agnes Kimwaga aliwataja wdau wengine watakaochangia kwenye kongamano hilo litakalongozwa na Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) Dkt. Herbet Makoye ambaye atakuwa Mwenyekiti.

Huku wajumbe na wazungumzaji watakuwa ni Bishop Hiluka (mwandishi na mtunzi), Harrieth Makweta (mwandishi), Wilson Makubi (Katibu Shirikisho la Filamu) Ado Novemba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Muziki, Edna Rajabu (TBC).

Naye Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, amesema kongamano hilo litafanyika Jumatatu ijayo Oktoba 15 katika Jukwaa la Sanaa kuanzia saa 4:30 asubuhi ambapo mada itakuwa ni ‘Mchango wa vyombo vya habari katika kudhibiti au kuchochea mmomonyoko wa maadili katika sekta ya sanaa’.

Ghonche amewakaribisha wadau wote ili kuleta michango, mapendekezo na hoja mbalimbali katika kuleta mustakabali utakaojenga sekta ya sanaa yenye maadili na itakayokuwa na tija kwa utamaduni wa taifa.

Hatua hivyo ya BASATA imekuja wiki moja baada ya kutoa maelekezo kwa mashirikisho ya sanaa kushughulikia suala la mmomonyoko wa maadili na kuwachukulia hatua wasanii wanaohusika na vitendo vya kujidhalilisha na kuidhalilisha tasnia ya sanaa na jamii kwa kuwa nusu utupu au kuandaa sanaa zinazokiuka maadili.

Post a Comment

0 Comments