WIZARA YA HABARI YAILIMA FAINI TFF YA SH.MIL5 YA UHARIBIFU U/TAIFA

  Pichani kulia ni  Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Leornad Thadeo,na Ofisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Lidya Churi.
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo imelilima faini ya sh.mil.5 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya urejeshwaji wa viti uliofanywa na mashabiki wanaodaiwa kuwa Simba katika mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF) baina ya Simba na Kiyovu uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Machi 4 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Leornad Thadeo,alisema, fedha hizo zitatumika kufanya ukarabati huo ambapo umeigiza TFF kuchunguza na kuwachukulia hatua wale waliohusika na vurugu hizo.

Alisema, Wizara inalaani kwa nguvu zote kitendo hicho ambacho kilitokana mashabiki wa Simba kwenda kukaa kwenye jukwaa walilokuwa wamekaa wale wa Yanga na mashabiki wengine hatua iliyosababisha tafrani uwanjani hapo.

Alifafanua kuwa jumla ya viti 152 viliharibiwa na 11 kuvunjwa kabisa tukio ambalo amelitaja kuwa lilileta fedheha kwa taifa.

Alisema, iwapo vitendo vya vurugu na uharibu wa mali vitaendelea Wizara italazimika kuufunga uwanja huo kwa muda ikiwa ni kuzuia kutokea kwa hali ya kuhatarisha maisha ya watu.
Thadeo, alisema, mashabiki wa soka wanapaswa kuwa wastaarabu na kutambua kuwa hali ya usalama uwanjani ni ya kila mmoja ikiwamo kuutunza uwanja huo uliojengwa kwa mabilioni ya fedha.

Post a Comment

0 Comments